Home / Michezo / Mourinho: Natumai Pogba anaelewa kwanini alicheza vizuri Urusi

Mourinho: Natumai Pogba anaelewa kwanini alicheza vizuri Urusi


Paul Pogba

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho ana matumaini kuwa Paul Pogba anaelewa kuhusu ni kwanini alicheza vizuri zaidi wakati wa mechi za Kombe la Dunia.

Kiungo hiyo wa safu ya kati wa Red Devils alifunga wakati Ufaransa waliishinda Croatia mabao 4-2 na kushinda Kombe la Dunia kwa mara ya pili.

Mourinho alisema Pogba mwenye miaka 25 alionyesha mchezo mzuri sana kwenye mechi tatu za mwisho nchini Urusi.

“Ni yeye mwenyewe kufahamu ni kwa nini alicheza vizuri, hasa wakati wa awamu ya pili ya mashindano,” alisema Mourinho.

Pogba alijiunga na United kwa pauni milioni 89 mwezi Agosti mwaka 2016, lakin akawa anachwa nje wakati wa mechi za msimu wa mwaka 2017-2018.

Aliachwa nje ya kikosi cha kwanza katika mechi zote wakati wa awamu za timu 16 za mwisho ambapo United ilishindwa na Sevilla.

Paul Pogba

Baada ya ushindi wa Ufaransa wa siku ya Jumapili beki wa zamani wa Manchester United Rio Ferdinand alisema “ni jukumu la Mourinho kumleta Pogba aliyekuwa kwenye Kombe la Dunia, alipitia mitihani migumu kwenye safu ya kati.

Huku Red Devil ikisafiri kwenda Marekani kwa safari ya maandalizi Pogba amebaki kupumzika.

Akizungumza huko Los Angeles, Mourinho alisema, “nilimfanyia Pogba kile nilichowafanyia wachezaji wengine.

Nilituma ujumbe mzuri kabla ya Kombe la Dunia na wakati wa Kombe la Dunia sikumsumbua yeyote, Walihitaji kuangazi tu kazi ya timu zao za kitaifa.

Mourinho alisema kipa David de Gea, kiungo wa kati Nemanja Matic na mchezaji mpya Fred watajiunga na kikosi hicho wiki ijayo.

Mshambuliaji Alexis Sanchez kujiuanga kwenye ziara hiyo baada ya kukosa kupata visa.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Nyota wa Afrika wamkumbuka mmiliki wa Leicester City Vichai Srivaddhanaprabha

Riyad Mahrez (kushoto) ni mmoja ya walitoa heshima zao kwa Vichai Srivaddhanaprabha Wachezaji wa Kiafrika …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *