Home / Afya / MAGONJWA YA DAMU YAUA WATU WENGI

MAGONJWA YA DAMU YAUA WATU WENGI

DAKTARI bingwa wa magonjwa ya damu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dar es Salaam, Stella Rwezaura amesema uelewa mdogo katika jamii unasababisha idadi kubwa ya watu kupoteza maisha kutokana na magonjwa ya damu.

Amesema moja ya magonjwa hayo ni himofilia ambao husababisha damu kukosa uwezo wa kuganda inayosababishwa na ukosefu wa kiwango cha kutosha cha chembechembe za protini zinazotakiwa kugandisha damu, hali inayosababisha damu kuvuja kwa muda mrefu.

Amesema mgonjwa anayekumbwa na hali hiyo, endapo hatapata huduma ya haraka anaweza kupoteza maisha.

Dk Stella amesema Watanzania wengi hawana utamaduni wa kupima afya zao, jambo linalosababisha watoto wengi kupoteza maisha hasa wale wanaopelekwa kwa waganga kukatwa kilimi au kutahiriwa.

“Utakuta mzazi anampeleka mtoto kumtahiri au kukata kilimi hajui ana tatizo la himofilia au hana, mtoto anatokwa damu nyingi mpaka anapoteza maisha au wale ambao wanaishi karibu na hospitali wanampeleka hospitali ameshatokwa na damu nyingi,” amesema.

Amesema kama kwenye familia kuna mtu ambaye alikuwa anatokwa na damu kwa muda mrefu, watoto wana uwezekano wa kurithi tatizo hilo ambalo ni himofilia, hivyo kabla ya kufanyiwa upasuaji wowote au hata kung’oa jino ni vizuri kupima uwezo wa damu kuganda.

Asilimia 97 ya wagonjwa wa himofilia hawajui kama wana ugonjwa huo na hawajawahi kupima.

Alisema wameshafanya mafunzo kwa waganga wa kienyeji wa jiji la Dar es Salaam pamoja na Pwani kuwafundisha ugonjwa huo, kwani watu wanaokwenda kwa waganga hao huchanjwa chale ambazo pia kama mtu ana himofilia anaweza kutoka damu mpaka akapoteza maisha.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

WANAWAKE WATAKIWA KUNYONYESHA WATOTO MAZIWA YAO PEKEE

WANAWAKE wametakiwa kunyonyesha watoto maziwa ya mama pekee bila kuwapa maji, kinywaji au chakula kingine …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *