Home / Afya / Kwa nini dawa za kuondoa maumivu zinazosababisha uraibu zinatumika?

Kwa nini dawa za kuondoa maumivu zinazosababisha uraibu zinatumika?


Dawa za Opioids husababisha uraibu iwapo matumizi yake yatakuwa kupita kiasi

Matumizi ya dawa za kuondoa maumivu za aina ya opioid zimeelezwa kuwa matumizi yake ya mara kwa mara yanasabisha uraibu wa dawa hizo,na hata wakati mwingine vifo.Hivyo kwa nini dawa hizi ambazo wakati mwingine ni hatari lakini bado wagonjwa hupatiwa dawa hizi?

Dawa za kundi hili ni miongoni mwa dawa zinazopendekezwa sana duniani kwa ajili ya kuondoa maumivu.

Dawa hizi-ikiwemo morphine,tramadol na fentanyl zinatumika kuondoa maumivu yanayosababishwa na kila kitu kuanzia matatizo ya moyo na saratani.

Lakini nchini Uingereza dawa hizi zimehusishwa na vifo vya mamia ya wagonjwa, wakati Marekani inapambana kudhibiti matumizi makubwa ya dawa hizo.

Kwa nini usitumie dawa nyingine za kuondoa maumivu ili kuepusha madhara?

Dawa hizi zinapotumika kwa wingi zinaweza kushusha kiwango cha upumuaji

Opioids ni dawa zinazofanya kazi kwa kiasi kikubwa na kwa ufanisi

Dawa hizi zinapotumika kwa wingi zinaweza kushusha kiwango cha upumuaji.

Uchunguzi uliofanyika katika Hospitali ya Gosport War Memorial umesema zaidi ya watu 450 walipoteza maisha kati ya mwaka 1989 na 2000 kutokana matumizi ya dawa hizo hatari bila maelekezo ya Daktari.

Nchini Marekani, kuongezeka kwa matumizi ya dawa za opioids kutibu maumivu ya muda mrefu yamesababisha uraibu wa dawa hizo.

Mwaka 2016, rekodi zinasema watu milioni 11.5 nchini Marekani walitumia dawa hizi kwa kukiuka masharti, hali iliyosababisha vifo vya 42,249 kutokana na kuzidisha dawa.

Kulikuwa na zaidi ya vifo vya watu 2000 nchini Uingereza vinavyohusiana na matumizi ya dawa hatari.Rekodi hii ni ya juu tangu utafiti ulipoanza.Lakini tofauti na vifo vilivyotokea Marekani, kwa kiasi kikubwa vilisabaishwa na dawa za kulevya, Heroin kuliko dawa za kundi la Opioids, zinazopatikana kwa maelezo ya daktari.

Sindano ikiwa kwenye pampu

Huleta ahueni kabisa

Moja ya sababu dawa hizi kutumika kwa wingi ni kuwa zinapotumika ipasavyo-zinafaa kuwa aina ya dawa ya kuondoa maumivu.Zinaweza kutumiwa na wagonjwa kwa namna mbalimbali na kwa njia tofautitofauti.

Morphine iko kwenye undi la opioids, mgonjwa anaweza kumeza au kupewa kwa kuchomwa sindano,kubandika au dawa za kuweka chini ya ulimi.

Ripoti ya Gosport ililenga njia ya kuingiza dawa ndani ya ngozi kwa kutumia pampu maalumu (Syringe drivers) ili kuruhusu kiasi sahihi cha dawa ya opioid kuingia mwilini kuondoa maumivu.

Pia pampu hizi humsaidia daktari kurekebisha kiasi cha dawa kinachohitajika mwilini.

Uraibu wa Tramadol wachochea machafuko Nigeria

Nilikuwa na uraibu wa kumeza vidonge 57 kwa siku

Pamoja na kuwepo kwa faida zake, matatizo yanayotokana na dawa hizi yanafahamamika

Kwa miongo kadhaa wanasayansi wamejaribu kutengeneza opioids ambazo zinaweza kufanya kazi bila usababisha matatizo ya uraibu na matumizi mabaya.

Wengine wameongeza viambato kwa makusudi , kwa mfano kuongeza dawa ya kupoza/kuondoa sumu, antidote naloxone ambazo kwa kiasi kikubwa hazina madhara

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

WANAWAKE WATAKIWA KUNYONYESHA WATOTO MAZIWA YAO PEKEE

WANAWAKE wametakiwa kunyonyesha watoto maziwa ya mama pekee bila kuwapa maji, kinywaji au chakula kingine …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *