Home / Afya / Madhara yakujichubuwa kwa Kumeza Vidonge

Madhara yakujichubuwa kwa Kumeza Vidonge

Watu wanaomeza vidonge vinavyobadili rangi mwili mzima na vipodozi vyenye kemikali, wapo kwenye hatari ya kupata magonjwa ya saratani.

Daktari Bingwa wa Ngozi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH),Dar es Salaam, Said Mwemba amesema hayo jijini Dar es Salaam.

Dk Mwemba amesema watu wa namna hiyo wanapotumia mara nyingi dawa na kemikali hizo, ngozi huathirika, na inapotengeneza vidonda hairudi katika hali ya kawaida.

“Ni kweli watu wanameza vidonge vinabadilisha rangi mwili mzima, kila kitu kinakuwa kilaini na mweupe. Ukitumia mara nyingi athari yake ni kubwa zaidi. Ngozi inaathirika ikitengeneza vidonda hairudi katika hali ya kawaida.

“Kama mtu hajatumia sana anaweza kurudi kwenye hali ya kawaida. Akipata magonjwa ya ngozi ambayo ngozi imeharibika inachukua muda kurudi katika hali ya kawaida na nyingi hazirudi. Ni vizuri mtu asijaribiwe kufanya vitu vya aina hiyo,” alisema Dk Mwemba.

Amesema vipodozi visivyofaa husababisha wembamba wa ngozi na mzio unaoleta matatizo kwa mtumiaji.

Ameshauri watu wanaotumia vitu hivyo kuacha kwa kuwa, vinaleta athari kubwa kwa kutengeneza vidonda ama chunusi.

“Unajua weupe unaleta urembo mtu anakuwa mrembo siku za mwanzo lakini urembo huo unaanza kuisha,” amesema na kuongeza kuwa hospitalini hapo kila siku hupokea mgonjwa mmoja au wawili wenye tatizo hilo la ngozi

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

WANAWAKE WATAKIWA KUNYONYESHA WATOTO MAZIWA YAO PEKEE

WANAWAKE wametakiwa kunyonyesha watoto maziwa ya mama pekee bila kuwapa maji, kinywaji au chakula kingine …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *