Home / Habari Za Kitaifa / Madiwani Chadema, CUF Wanaswa Baa

Madiwani Chadema, CUF Wanaswa Baa

Madiwani wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na mmoja wa Chama cha Wananchi (CUF) Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam wamekamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wakidaiwa kupokea rushwa ya Sh milioni tatu ili kumpitisha mzabuni wa ujenzi wa soko la kisasa la Kisutu.

Madiwani hao ni Edwin Mwakatobe ambaye ni wa Kata ya Segerea, Shukuru Abdalah Dege wa kata ya Mnyamani na Joseph Ngowa ambaye ni Diwani wa kata ya Mchikichini.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Ilala, Zainabu Bakari jana, madiwani hao walikamatwa katika Bar ya Kwetu Pazuri iliyoko Tabata katika wilaya hiyo baada ya kuwekewa mtego.

“Mnamo Julai 24 mwaka 2018 Takukuru Mkoa wa Ilala iliwakamata madiwani watatu katika mtego wa rushwa kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa ya shilingi milioni tatu,” imesema taarifa hiyo.

Amesema kosa hilo ni kinyume na kifungu cha sheria 15 (1)(a) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11/2007.

Aidha, madiwani hao walipokea fedha hizo ili waweze kumpitisha mzabuni mtaalamu mshauri katika usimamizi wa ujenzi wa soko la kisasa la Kisutu litakalogharimu kiasi cha Sh bilioni 13.4.

Uchunguzi wa tuhuma hizo unaendelea, watuhumiwa wako nje kwa dhamana na watafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Historia ya marehemu Isaac Nyagabona Muyenjwa Gamba

HISTORIA YA MAREHEMU ISAAC NYAGABONA MUYENJWA GAMBA. Ratiba Kwa Ufupi Jumatatu Alfajiri – Kupokea Mwili Airport …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *