Home / Afya / Wiki ya kimataifa ya kunyonyesha mtoto: Zifahamu faida za kunyonyesha

Wiki ya kimataifa ya kunyonyesha mtoto: Zifahamu faida za kunyonyesha


Tamaduni nyingi zisizomruhusu mwanamke kunyonyesha maeneo ya umma pia ni changamoto kwa wanawake wanaonyonyesha

Wakati ulimwengu ukiadhimisha wiki ya kimataifa ya kunyonyesha mtoto na kuelezea faida zake kwa wazazi na taifa, wakazi wa dunia wanahamashishwa kufahamu umuhimu wa maziwa ya mwanzo kabisa ya mama kwa mtoto .

Takriban 40% tu ya watoto wachanga wenye umri kati ya miezi 0 hadi 6 ndio wanaoishi kwa kunyonyeshwa pekee, kulingana na shirika la Shirika la Afya duniani.

Kadhalika shirika hilo linasema kuwa zaidi ya maisha ya watoto 820 000 walio na umri wa chini ya miaka 5 yanaweza kunusurika kila mwaka, ikiwa watoto wenye umri kati ya if all miezi 0 hadi 23 wangenyonyeshwa kikamilifu.

Ukweli kuhusu umuhimu wa kunyonyesha:

 • Kunyonyesha ni moja ya njia sahihi ya kuhakikisha mtoto anakuwa mwenye afya na kuendelea kuishi.
 • Kama viwango vya kunyonyesha vingekuwa vya hali ya juuduniani , takriban maisha 820 000 ya watoto yangenusurika kila mwaka, linasema shirika la afya duniani (WHO).
 • Unyonyeshaji wa mtoto kwa miezi 6 kuna faida nyingi za kiafya kwa mama na mtoto.
 • Kumnyonyesha mtoto mara anapozaliwa kwa kipindi cha saa moja, humkinga kwa maambukizi yanayowapata watoto wachanga na kupunguza vifo vya watoto wachanga.
 • Maziwa ya mama pia ni chanzo muhimu cha nguvu na virutubisho kwa watoto wa kati ya miezi 6 hadi 23.
 • Maziwa ya mama yanaweza kuchangia nusu au zaidi ya nguvu za mtoto katika umri wa miaka 6 hadi 12
 • Watoto na vijana wadogo walionyonyeshwa wakiwa wachanga wana uwezekano mdogo wa kuwa na uzito wa mwili wa kupindukia .
 • Unyonyeshaji wa mtoto humsaidia kuboresha uwezo wa utambuzi wa akili (IQ), mahudhurio ya shule , na pia huhusishwa na mapato ya juu katika maisha yake ya utu uzima.
 • Kunyonyeshwa kwa muda mrefu pia huchangia afya na maisha bora ya mama kwani humpunguzia hatari ya kupata saratani ya mfuko wa mayai ya uzazi na matiti.
 • Kunyonyesha hutengeneza vichocheo vyamwili( hormone) ambazo humtuliza mama na mtoto

Juma hili linaadhimishwa huku baadhi ya wanawake duniani wakishindwa kuwanyonyesha watoto wao ipasavyo kutokana na sababu mbali mbali. .

Takriban 40% tu ya watoto wachanga wenye umri kati ya miezi 0 hadi 6 ndio wanaoishi kwa kunyonyeshwa pekee, kulingana na shirika la Shirika la Afya duniani

Licha ya juhudi mbali mbali ambazo zimekuwa zikifanyika kuelemisha wakina mama na jamii nzima juu ya umuhimu wa kunyonyesha na maziwa ya mama kwa mtoto, baadhi ya mila na tamaduni hususan za Kiafrika zimekuwa na changangoto kubwa ya kuelewa na kukubali umuhimu wa kunyonyesha kutokana na kukosa elimu ya kunyonyesha.

Miongoni mwa changamoto zinachangia wanawake kushindwa kuwanyonyesha watoto wao ni pamoja na kazi, magonjwa pamoja na tamaduni nyingi zisizomruhusu mwanamke kunyonyesha maeneo ya umma.

Hivi karibuni mwanamke mmoja nchini Kenya alifukuzwa kwenye mgahawa jijini Nairobi alipokuwa akimnyonyesha mwanae ndani ya mgahawa huo.

Aidha baadhi yao wamekuwa na imani potofu kuhusu suala zima la kunyonyesha na faida zake. Hili limechangia pakubwa katika kudhoofisha jitihada za kuhakikisha kila mama mwenye mtoto mchanga anamyonyesha ipasavyo.

Baadhi ya imani potofu kuhusu kunyonyesha:

 • Maziwa ya kwanza ya mama si mazuri kwa mtoto yanapaswa kumwagwa
 • Kunyonyesha humfanya mama anenepe kupindukia
 • maziwa ya mama pekee hayawezi kumridhisha mtoto wa umri wa miezi 0 hadi sita.
 • Baadhi ya vyakula si vizuri kwa wanawake wanaonyonyesha
 • Ni lazima mtoto mchanga anywe maji mara baada ya kuzaliwa
 • Maziwa ya mama humfanya mtoto ajihisi mwenye kiu
 • Baadhi ya wanawake hudai wanaponyonyesha matiti yao husinyaa na kuanguka.

Shirika la watoto la Save the Children linasema kuwa watoto wenye utapiamlo unaochangiwa na kutonyonyeshwa ipasavyo unakadiriwa kusabisha vifo vya watoto 2.7 kila mwaka.

 

Aliya Shagieva akimnyonyesha mwanae, Wataalam wanasema mguso wa mwili baina ya mama na mtoto wakati wa kunyonyesha husaidia kuchochea uzalishaji wa maziwa ya mama

Wiki ya kimataifa ya kunyonyesha inaadhimishwa huku serikali na wakazi wa dunia kwa ujumla wakitolewa wito kuwasaidia wanawake kuwanyonyesha watoto katika kipindi cha saa moja ya kwanza ya uhai wake.

Wataalam wanasema mguso wa mwili kwa mwili pamoja na kunyonya husaidia kuchochea uzalishaji wa maziwa ya mama , yakiwemo maziwa ya mwanzo kabisa ya mama baada ya kujifungua ambayo hutambuliwa kama”chanjo ya kwanza” , yenye virutubisho vingi pamoja na kinga ya ya mwili.

Huenda ukavutiwa na taarifa hizi nyingine pia:

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

WANAWAKE WATAKIWA KUNYONYESHA WATOTO MAZIWA YAO PEKEE

WANAWAKE wametakiwa kunyonyesha watoto maziwa ya mama pekee bila kuwapa maji, kinywaji au chakula kingine …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *