Home / Afya / Mtoto mwenye siku 12 ang’olewa jino

Mtoto mwenye siku 12 ang’olewa jino


Mama yake Isla-Rose anasema ”hakutarajia” kumpeleka mwanae kwa daktari wa meno akiwa na umri mdogo

Mtoto mchanga wa kike aliyezaliwa akiwa ameota jino moja ameng’olewa jino hilo akiwa na siku 12.

Mama wa Isla-Rose Heasman, Jasmin kutoka Plymouth Devon nchini Uingereza, alisema ”hakutegemea” kuwa angempeleka binti yake kwa daktari wa meno katika umri mchanga.

”Ilibidi atolewe jino, ilikuwa inaogopesha.Alikuwa jasiri kuliko mimi, hakulia kabisa,”Alieleza

Kituo hicho cha tiba ya meno kimesema kuwa Isla-Rose ni ”mgonjwa mwenye umri mdogo zaidi” kuwahi kutokea, na alipatiwa beji kama zawadi

Watoto wengi huota meno wanapofikia umri wa miezi sita wengine wakiwa na miezi na wengine mpaka baada ya mwaka mmoja.

Isla-Rose alipatiwa dawa ya kumkinga na maumivu kabla ya kutolewa jino, alipatiwa zawadi kwa kuwa alikuwa jasiri

”Ilinibidi nitoke nje ya chumba nikiwa nalia kwa sababu sikuweza kuvumilia kutazama mwanangu akiwa katika maumivu.

Daktari wa meno alimpatia Isla-Rose zawadi ya karatasi yenye maandishi kama zawadi ya kuwa shujaaa

Kwa mujibu wa shirikisho la wataalamu wa afya ya meno nchini humo,BDA, takriban mtu mmoja kati ya 2000 huzaliwa wakiwa na jino.

Huwa yanalegea kwa sababu mizizi ya meno inakuwa bado haijaimarika.

Profesa Damien Walmsley, anasema: ”hali hiyo inaweza kusababisha matatizo ya kunyonyesha,ulimi wa mtoto kupata vidonda, na hatari ya jino kuchomoka na kuingia kwenye mapafu ya mtoto.Hata hivyo changamoto hizi ni nadra kutokea

Jino lilitolewa na kuwekwa kwenye mkebe kwa ajili ya familia kwenda nalo nyumbani

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

WANAWAKE WATAKIWA KUNYONYESHA WATOTO MAZIWA YAO PEKEE

WANAWAKE wametakiwa kunyonyesha watoto maziwa ya mama pekee bila kuwapa maji, kinywaji au chakula kingine …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *