Home / Habari Za Kitaifa / WALE WA ‘NITUMIE FEDHA HUMU’ KORTINI

WALE WA ‘NITUMIE FEDHA HUMU’ KORTINI

WATU 13 wanaodaiwa kutuma ujumbe wa maandishi kuomba kutumiwa fedha, wamefi kishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashitaka ya uhujumu uchumi ikiwemo utakatishaji fedha wa Sh milioni 154.

Washitakiwa hao; ni Boniface Maombe, David Luvanda, Moshi Sungura, Amos Bosco, Lule Kadenge, Jofrey Kapangamwaka, William Nturo, Regius Mauka, Collins Basham, Francis Kapalata, Kasonde Kapela, Enock Mwandaji na Pascal Kiatu ambao walifikishwa mahakamani hapo jana.

Akisoma mashitaka hayo, Wakili wa Serikali Mkuu, Nassoro Katuga alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Kelvin Mhina kuwa washitakiwa hao wanakabiliwa na mashitaka matano waliyoyatenda katika mikoa tofauti ya Dar es Salaam na Rukwa.

Katuga alidai katika mashitaka ya kwanza kuwa kati ya Machi na Juni mwaka huu, maeneo ya Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa Rukwa na maeneo mengine ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, washitakiwa walikula njama kutenda kosa hilo.

Pia alidai kati ya Machi na Juni mwaka huu, wakiwa Dar es Salaam na Rukwa washitakiwa hao walichapisha na kusambaza taarifa za uongo za ujumbe mfupi wa maandishi kwa kutumia mfumo wa kompyuta ili kujipatia fedha.

Wakili Katuga alidai mashitaka mengine ni kusambaza jumbe kwa njia ya kielektroniki walilolitenda kati ya Machi na Juni, mwaka huu, maeneo ya Dar es Salaam na Rukwa ambapo inadaiwa kwa nia ya kudanganya na kushawishi, walisambaza kwenda kwa watu tofauti tofauti jumbe hizo ili kuonyesha wana mamlaka hayo.

Pia wanadaiwa kati ya Machi na Juni mwaka huu, maeneo ya Dar es Salaam na Rukwa walisambaza jumbe zisizotakiwa kwa njia ya kielektroniki. Katika mashitaka ya tano, inadaiwa katika miezi hiyo hiyo, mwaka huu na katika maeneo ya Dar es Salaam na Rukwa kwa pamoja walijihusisha katika ufanyaji wa muamala wa Sh milioni 154,032,830 ikiwa ni zao la kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Aidha, Wakili Katuga alidai kuwa upelelezi wa shauri hilo haujakamilika. Hakimu Mhina alisema kesi hiyo haina dhamana kwa sababu mashitaka ya uhujumu ni ya uchumi, hivyo aliamuru washitakiwa warudishwe rumande hadi Agosti 21, mwaka huu kesi itakapotajwa tena.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Historia ya marehemu Isaac Nyagabona Muyenjwa Gamba

HISTORIA YA MAREHEMU ISAAC NYAGABONA MUYENJWA GAMBA. Ratiba Kwa Ufupi Jumatatu Alfajiri – Kupokea Mwili Airport …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *