Home / Habari za Kimataifa / Mwanasiasa wa Zimbabwe Tendai Biti anyimwa hifadhi Zambia

Mwanasiasa wa Zimbabwe Tendai Biti anyimwa hifadhi Zambia


Biti alikuwa ni waziri wa fedha kwenye serikali ya umoja iliyobuniwa baada ya uchaguzi uliokumbwa na utata wa mwaka 2008 na ilisifiwa kwa kusaidia kuboresha uchumi.

Mwanasiasa wa cheo cha juu kwenye muungano wa upinzani nchini Zimbabwe MDC Tendai Biti amenyimwa hifadhi kwenye taifa jirani la Zambia.

Polisi wa Zimbabwe wanamlaumu Bw Biti kwa kuchochea ghasia kufuatia uchaguzi wa mwezi uliopita.

Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Zambia Joe Malanji aliiambia BBC kuwa vigezo vya vyake kuomba hifadhi vilikuwa dhaifu.

Alizuiwa eneo salama hadi pale aliporejeshwa Zimabwe, waziri alisema.

Mapema wakili wake alisema mteja wake alikuwa amezuiwa kwenye mpaka na Zambia na mamlaka za Zimbabwe.

Ripoti zingine za polisi wa Zambia zinazo sambaa kwenye mitandao ya kijamii zinasema kuwa maafisa wa Zimbabwe walijaribu kumkamata Bw Biti baada ya yeye kuvuka na kuingia Zambia.

Mwanasiasa huyo wa upinzani akaomba msaada kwa sauti na karibu ya wasafiri 300 wa Zimbabwe wakawazuia maafisa wa usalama wa seriali kumkamata, kulingana na ripoti.

Maafisa wa Zambia kisha wakaingilia kati na kutishia kuwakamata maafisa wa Zimbabwe kwa kujaribu kutekeleza wajibu wao ndani ya ardhi ya Zambia.

Tendai Biti is wanted in connection with the post-election violence that left six people dead after opposition supporters clashed with soldiers

Kulikuwa na matumaini kuwa uchaguzi wa mwezi Julai ungeleta mabadiliko makubwa baada ya kumalizika kwa utawala wa Rais Robert Mugabe Novemba iliyopita.

Lakini wiki iliyopita watu 6 waliuawa baada ya jeshi kuingilia kati kuzima maandamano ya upinzani kwenye mji mkuu Harare.

Waandishi wa habari wanasema kuna hali ya hofu nchini Zimbabwe huku baadhi ya wanachama wa upinzani wakiingia mafichoni.

Tume ya uchaguzi ilitangaza kuwa Rais Emmerson Mnangagwa alishinda uchaguzi lakini muungano wa MDC unadaia kuwa uchaguzi uliibwa.

Upinzani unasema mgombea wake Nelson Chamisa alikuwa ndiye mshindi na matokeo yalikarabatiwa

Biti alikuwa ni waziri wa fedha kwenye serikali ya umoja iliyobuniwa baada ya uchaguzi uliokumbwa na utata wa mwaka 2008 na ilisifiwa kwa kusaidia kuboresha uchumi.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mohamed Bin Salman

CIA ‘yamlaumu mwanamfalme wa Saudia ‘

Shirika la ujasusi la Marekani(CIA) linaamini kuwa Mwanamfalme Mohammed bin Salman wa Saudi Arabia ndiye …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *