Home / Habari za Kimataifa / Shambulizi la Skripal: Marekani kuiwekea vikwazo Urusi, kuanzia Agosti

Shambulizi la Skripal: Marekani kuiwekea vikwazo Urusi, kuanzia Agosti


Sehemu ya mji wa Salisbury ilizingirwa kuzuia kusambaa kwa kemikali hiyo

Marekani imepanga kuweka vikwazo vipya kwa Urusi ikiwa ni kujibu kitendo cha shambulizi la sumu la afisa wa zamani wa usalama wa Urusi Sergei Skripal na mtoto wake wa kike nchini Uingereza.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Marekani Heather Nauert, amesema nchi yake imegundua kuwa Urusi ilitumia kemikali hatari kumshambulia Skripal na binti yake wa kike jambo ambalo ni ukiukwaji wa sheria za kimataifa.

Hii ni mara ya tatu Marekani inaiwekea vikwazo nchi fulani kwa kukiuka sheria hii.

Polisi iliweka vizuizi sehemu zote

Serikali ya Uingereza imeunga mkono suala hilo.

Urusi mara kwa mara imekua ikikanusha tuhuma hizi.

Vikwazo hivi vinatarajiwa kuaza mwishoni mwa mwezi Agosti.

Skripal na binti yake Yulia walikutwa wamepoteza fahamu baada ya shambulizi hilo

Katika taarifa iliyotolewa Jumatano , wizara ya mambo ya nje ya Marekani ilithibitisha kuchukua hatua dhidi ya Urusi kuhusiana na tukio la uvamizi kwa kutumia sumu ya kemikali kwa Sergei Skripa na binti yake lililofanyika nchini Uingereza.

Msemaji wa wizara hiyo Heather Nauert amesema imegundulika kuwa Urusi ilitumia sumu hiyo kinyume cha sheria za kimataifa.

Serikali ya Uingereza imeopongeza hatua hiyo kwa kusema ilistahili kwa nchi ambayo inatabia zisizo za kiungwana na ambazo hazivumuliki.

Wanausalama wa Uingereza wakijizuia na sumu hiyo

Vikwazo hivyo vipya vinatarajia kuanza Agosti 22 vikigusia zaidi uzuiaji wa vifaa vya umeme na teknolojia nyingine kwenda na kutoka Urusi.

Marekani inasema vikwazo vingine vingi zaii vinatarajia kufuata iwapo Urusi itashindwa kuuthibitishia ulimwengu kuwa itaacha mara moja matumizi ya kemikali za aina hiyo.

Hii ni mara ya tatu Marekani kuweka vikwazo kwa nchi iliyotumia kemikali katika mashambulizi dhidi ya binaadam, ikifanya hivyo kwa Syria na Korea Kaskazini.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mohamed Bin Salman

CIA ‘yamlaumu mwanamfalme wa Saudia ‘

Shirika la ujasusi la Marekani(CIA) linaamini kuwa Mwanamfalme Mohammed bin Salman wa Saudi Arabia ndiye …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *