Home / Habari Za Kitaifa / HOSPITALI 24 ZANZIBAR KUUNGANISHWA MKONGO WA TAIFA

HOSPITALI 24 ZANZIBAR KUUNGANISHWA MKONGO WA TAIFA

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) inakamilisha mpango wa kuunganisha hospitali 24 katika Mkongo wa Taifa kwa lengo la kuboresha utoaji wa huduma za afya.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Teknolojia (Tehama) wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa SMZ, Dk Mzee Suleiman Mndewa wakati akizungumza na waandishi wa habari waliofanya ziara ya kujifunza na kuona maendeleo ya Tehama yalivyobadilisha taswira ya uchumi wa Zanzibar.

Dk Mndewa alisema uunganishaji hospitali katika Mkongo wa Taifa ni sehemu ya mpango wa utoaji huduma za afya kwa mfumo unaojulikana kama e-health, ikiwa ni utekelezaji wa azma ya SMZ ya kutumia teknohama katika kuboreha huduma za kijamii.

“Baada ya kumaliza ujenzi wa Mkongo wa Taifa, serikali sasa inajenga maeneo ya kuwezesha upatikanaji wa mtandao huo ili uweze kuzifikia taasisi zote za serikali.

“Ujenzi wa kanzidata kwa ajili ya e-health umekamilika na kinachoendelea hivi sasa ni zoezi la kupakia takwimu za afya kutoka hospitali hizo katika mfumo wenyewe,” amesema Dk Mndewa.

E-health ni mfumo unaowawezesha mawasiliano kuhusu taarifa za mgonjwa kati ya wataalamu wa afya. Mfumo huo pia hurahisisha zoezi la kufanya vipimo, majibu yake (ya vipimo) na tiba kwa wagonjwa.

Wataalamu wa afya pia huwasiliana kuhusu mbinu mbalimbali za jinsi ya kuweza kubaini chanzo cha matatizo na tiba sahihi kwa wagonjwa kupitia mfumo wa e-health.

Kwa mujibu wa Dk Mndewa, mfumo wa teknohama utaunganishwa pia katika katika biashara kama zile za hoteli na biashara nyingine ili kuchochea uanzishwaji wa shughuli nyingine za uzalishaji, kama vile vipindi vya kwenye runinga miongoni mwa Wazanzibari.

“Lengo la Mkongo wa Taifa ni kulisaidia taifa kutambua kwamba manufaa ya teknohama huenda mbali zaidi ya matumizi ya kawaida ya intaneti na kwamba ikitumika vizuri, itachochea uzalishaji haswa katika nyanja za ubunifu wa vipindi vya kwenye runinga vitakavyotumika nchini kote,” amesema.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Historia ya marehemu Isaac Nyagabona Muyenjwa Gamba

HISTORIA YA MAREHEMU ISAAC NYAGABONA MUYENJWA GAMBA. Ratiba Kwa Ufupi Jumatatu Alfajiri – Kupokea Mwili Airport …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *