Home / Michezo / MTIBWA YAPATA MRITHI WA DILUNGA

MTIBWA YAPATA MRITHI WA DILUNGA

BAADA ya Simba SC kumnyakua kiungo wa Mtibwa Sugar, Hassan Dilunga, tayari kocha wa timu hiyo Zuberi Katwila amepata mtu wa kuziba pengo lake.

Dilunga ambaye alishawahi kuichezea Yanga, amejiunga na Simba kwa mkataba wa miaka miwili anatarajiwa kuipa mafanikio makubwa timu hiyo kwenye mechi za Ligi Kuu, FA pamoja na mechi za Klabu Bingwa Afrika.

Akizungumza na gazeti hili jana, Katwila alisema, kuondoka kwa Dilunga hakutakiathiri kikosi chake kwani tayari ameshapata mrithi wa kuziba pengo lake.

Alisema kuwa timu yake ina wachezaji wengi akiwemo Ayub Semtawa na Saleh Hamis ambao wanaimudu vema nafasi hiyo ya kiungo.

“Haikuwa kazi ngumu kumpata mtu atakayeziba nafasi yake kwani hata kipindi ambacho alikuwepo alikuwa akipokezana na Semtawa hivyo naweza kusema nafasi yake wapo watu wa kuiziba.

“Kama kocha makini unapokuwa na timu yako lazima uwe na wachezaji mbadala kama ataondoka mmoja basi unamuweka mwingine bila kutetereka,” alisema Katwila.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Nyota wa Afrika wamkumbuka mmiliki wa Leicester City Vichai Srivaddhanaprabha

Riyad Mahrez (kushoto) ni mmoja ya walitoa heshima zao kwa Vichai Srivaddhanaprabha Wachezaji wa Kiafrika …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *