Home / Habari za Kimataifa / Kesi ya talaka: Brad Pitt ajibizana na Angelina Jolie kuhusu gharama ya malezi ya watoto

Kesi ya talaka: Brad Pitt ajibizana na Angelina Jolie kuhusu gharama ya malezi ya watoto


Wasanii hao wa Hollywood walikuwa wapenzi tangu 2005 lakini walifunga ndoa 2014

Mwigizaji maarufu kutoka Marekani Brad Pitt amepuuzilia mbali tuhuma zilizotolewa na mke wake waliyetengana Angelina Jolie kwamba amewatelekeza watoto wake.

Katika nyaraka za kujibu kesi Jumatano, mawakili wa mwigizaji huyo wanasema kwamba amelipa jumla ya $1.3m (£1m) kama gharama ya malezi ya watoto wake na kwamba amemkopesha Jolie jumla ya $8m kumsaidia kununua nyumba.

Jumanne, wakili wa Jolie alidai kwamba Pitt hajatoa mchango wowote wa maana wa kusaidia kuwalea watoto wao tangu Jolie alipowasilisha kesi ya kuomba talaka mwaka 2016.

Wawili hao walikuwa wameishi pamoja kama mume na mke tangu 2005 lakini walifunga ndoa mwaka 2014.

Kwenye nyaraka za kujibu tuhuma za upande wa Jolie, mawakili wa Pitt wamesema madai ya mwanamke huyo kuhusu gharama ya malezi ya watoto “yameandaliwa na kutolewa mahsusi kuelekeza mtazamo wa vombo vya habari.”

Kufikia sasa upande wa Jolie bado haujajibu tuhuma hizo za Pitt.

“[Pitt] ana wajibu wa kisheria wa kuchangia utunzaji wa watoto. Kufikia sasa, [yeye] hajatoa mchango wowote wa kuwatunza watoto tangu walipotengana (na Jolie),” wakili wa Jolie alisema kwenye nyaraka za mahakama Jumanne.

Uhusiano ulipokuwa bado imara

“Ikizingatiwa kwamba makubaliano yasiyo rasmi kuhusu malipo ya gharama ya watoto hayajaendelezwa… kwa mwaka mmoja unusu sasa [Jolie] anakusudia kuwasilisha ombi la kutolewa kwa agizo la kumlazimisha Pitt kulipa gharama ya watoto,” nyaraka hizo za mahakama zinasema.

Jolie alisema kumetokea tofauti ambazo haziwezi kusuluhishwa alipowasilisha ombi la kutaka talaka.

Wawili hao walizozana kuhusu nani awe na watoto kwa miezi kadha baada ya tangazo hilo kutangazwa.

Pitt alichunguzwa kuhusiana na uwezekano kwamba aliwadhalilisha watoto wake baada yake kupoteza subira akiwa mbele ya watoto hao.

Lakini baadaye aliondolewa makosa hayo.

Wawili hao walifahamika sana kama “Brangelina” na mashabiki wao na walikutana wakiigiza filamu ya Mr and Mrs Smith ya mwaka 2005.

Harusi hiyo ilikuwa ya pili kwa Pitt, kwanza alikuwa amemuoa mwigizaji nyota Jennifer Aniston.

Kwa Jolie, hiyo ilikuwa harusi yake ya tatu, baada ya ndoa yake na Billy Bob Thornton na nyingine na Jonny Lee Miller.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mohamed Bin Salman

CIA ‘yamlaumu mwanamfalme wa Saudia ‘

Shirika la ujasusi la Marekani(CIA) linaamini kuwa Mwanamfalme Mohammed bin Salman wa Saudi Arabia ndiye …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *