Home / Habari Za Kitaifa / UJENZI STENDI, SOKO KUAJIRI WATU 500

UJENZI STENDI, SOKO KUAJIRI WATU 500

MRADI wa Ujenzi wa Kituo Kikuu cha Mabasi na Soko la Kisasa jijini Dodoma unategemewa kuzalisha ajira zaidi ya 500 zitakazowanufanisha wakazi wa jiji la Dodoma.

Hayo yalielezwa na Mkurungenzi wa Kampuni ya Mohammed Builders inayojenga soko na stendi jijini Dodoma, Mohammed Jafferji wakati akizungumza katika eneo la ujenzi wa miundombinu hiyo.

Jafferji alisema miradi hiyo miwili itanufaisha na ujenzi wa miradi hiyo inayojengwa katika eneo la Nzuguni na hivyo kuongeza fursa ya ajira mkoani humo.

“Hatuwezi kuchukua watu wa kazi kutoka mbali tutatoa kipaumbele kwa wananchi walipo hapa jirani kwanza ili waweze kunufaika na uwepo wa miradi hii miwili,” alisema Jafferji.

Alisema pamoja na ajira za moja kwa moja pia miradi hiyo itanufaisha watu wengine kama mamalishe ambao watakaotoa huduma ya chakula kwa wafanyakazi wa miradi hiyo.

Hata hivyo Jafferji alisema, kampuni hiyo inatekeleza ujenzi wa kituo cha mabasi pamoja na ujenzi wa soko jipya la kisasa katika eneo la Nzuguni na wanatakiwa kukamilisha ndani ya miezi 15 na utakamilika mwezi Septemba, mwakani.

Alisema walifanya mkutano na wananchi wa eneo hilo la Nzuguni na kukubaliana kupata watu wakazi wa eneo hilo ili kunufaika na uwepo wa miradi hiyo.

Alisema kwa sasa kampuni hiyo imeanza hatua za awali za ujenzi kwa kuchimba mashimo ya nguzo za jengo kuu, lakini hatua inayofuata ni kuanza ujenzi na hadi sasa hawajapata changamoto ya kuibiwa vifaa vya kazi kutokana na wenyeji kushiriki katika ulinzi wa vifaa hivyo.

Mkazi wa Nzuguni, Yohana Matonya aliishukuru kampuni hiyo kwa kuona umuhimu wa kuwapa kipaumbele wakazi hao katika kuwapa ajira.

Alisema anaamini uwepo wa miradi hiyo katika eneo la Nzuguni watanufaika kwa kujengewa miundombinu ya barabara pamoja na kupata faida ya kusogezewa huduma nyingine karibu na eneo lao.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Historia ya marehemu Isaac Nyagabona Muyenjwa Gamba

HISTORIA YA MAREHEMU ISAAC NYAGABONA MUYENJWA GAMBA. Ratiba Kwa Ufupi Jumatatu Alfajiri – Kupokea Mwili Airport …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *