Home / Habari Za Kitaifa / UDOM KUDAHILI KWA MTANDAO

UDOM KUDAHILI KWA MTANDAO

IDARA ya Teknolojia ya Mawasiliano (IT) ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) imesema wanafunzi wa mwaka huu wa 2018/19 watadahiliwa kwa kutumia mfumo wa mtandao.

Akizungumza kwenye Maonesho ya Nanenane Nzuguni jijini hapa, mtaalamu IT wa Udom, Jane Mbuligwe alisema udahili huo unafanyika kwa haraka pungufu ya dakika 20.

Alisema wanafunzi hayo walioomba udahili wa kusoma kozi mbalimbali chuoni hapo, ni wale wanaotaka kusoma shahada za kwanza bila kuchanganya wanaotaka kusoma stashahada na astashahada ambao wameomba 5,000.

Mbuligwe alisema ili kuwapata wanafunzi 15,000 wanaotakiwa kuanza masomo mwaka huu 2018/19, mtandao wenyewe utachuja na kubaki wanaostahili, vigezo na taaluma inayotakiwa, kuanza kozi chuoni hapo mwezi Oktoba.

“Waliotuma maombi watachujwa na mfumo wenyewe kulingana na vigezo vilivyowekwa ili kupata wanafunzi 15,000 ambao wanatakiwa kuanza kozi za shahada mbalimbali katika mwaka huu wa masomo,” alisema.

Alisema kutokana na mafanikio makubwa chuo kinayopata tangu kuanzishwa kwake 2007, anawataka wazazi wenye watoto wenye sifa watumie fursa ya uwepo wa chuo hicho kusoma kozi mbalimbali zinazotolewa chuoni hapo.

Ofisa anayeshughulikia usajili wa wanafunzi chuoni hapo, Suzan Mayengo alisema chuo hicho, kinatoa elimu bora na ndiyo maana kimeweka banda hapo Nanenane ili kutoa elimu kwa wakulima, wavuvi na wafugaji kuhakikisha kinatumia taaluma katika kuzalisha bidhaa zao.

Mhadhiri wa chuo hicho, Dk Emmanuel Ishengoma alisema wameweka banda na wamekuwa wakishiriki katika maonesho ya Nanenane kila mwaka ili kueleza umuhimu wa taaluma katika kuboresha kilimo, uvuvi na ufugaji.

Dk Ishengoma alisema ili kudumisha kilimo, uvuvi na ufugaji bora lazima wahusika wawe na taarifa sahihi, lakini pia wawe na afya njema kwa kupima bure katika banda hilo lakini pia wapate taaluma kutokana na miradi ya wanafunzi ambayo inalenga kuwapa elimu ya kupata tija na kuleta maendeleo ya viwanda.

Mwanafunzi wa Udom, Pius Mwikola ambaye amegundua mfumo wa ulinzi, alisema taaluma hiyo ya kulinda mali za wakulima, wavuvi na wafugaji ni muhimu kwani kupitia simu za mikononi mkulima atapata taarifa kuhusu wanyama waharibifu walioingia shambani mwake.

Chuo Kikuu cha Dodoma kimekuwa kikishiriki katika maonesho ya Nanenane yanayofanyika katika viwanja vya Nzuguni jijini hapa, lengo ni kuwapa elimu watu mbalimbali namna ambavyo wanahitaji taaluma katika kuzalisha na kutoa huduma.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Historia ya marehemu Isaac Nyagabona Muyenjwa Gamba

HISTORIA YA MAREHEMU ISAAC NYAGABONA MUYENJWA GAMBA. Ratiba Kwa Ufupi Jumatatu Alfajiri – Kupokea Mwili Airport …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *