Home / Habari Za Kitaifa / Picha WAZIRI AWAWAKIA WANAOJICHIMBIA VISIMA BILA VIBALI, WAKAIDI TOZO ZA MAJI

Picha WAZIRI AWAWAKIA WANAOJICHIMBIA VISIMA BILA VIBALI, WAKAIDI TOZO ZA MAJI

WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa amewataka wadau wote wanaotumia maji kulipa tozo za maji kama sheria ya usimamizi wa raslimaliza maji Namba 11 ya mwaka 2009, inavyoelekeza.

Aidha amewataka wananchi wote kuhakikisha kabla hawajachimba kisima cha maji kuhakikisha wanapata vibali kutoka kwenye mamlaka husika na kwa kuwa wengi wameonekana kuchimba bila kufuata sheria na taratibu.

Profesa Mbarawa ameyasema hayo leo, Jumatatu, jijini Dar es Salaam katika kikao cha kujadili tozo mpya za matumizi ya maji amacho kimewaleta pamoja wajumbe wa bodi ya Shirikisho la Wamiliki wa Viwanda nchini na wadau wa sekta ya maji ulioandaliwa na Bonde la Wami/Ruvu.

“Nilitembelea Ofisi za Bonde wiki mbili zilizopita na nikauliza utaratibu wa kutoa vibali kwa ajili ya watu wanaochimba visima vya maji na katika kupitia nikakuta pameandikwa watumiaji wa maji haswa wenye viwanda wanatakiwa kulipa Sh kwa lita moja na nikauliza wanalipa nikaambiwa wamekuwa wagumu kulipa,”  Waziri amesema na kuongeza “nilipoona hivyo nikasema hawa watu nawafahamu hebu tukae tujadiliane kwa maslahi ya maji na Taifa letu, siamini Mtanzania yeyote akiambiwa afanye kazi kwa maslahi ya nchi yake atakataa.”

Amesema kuwa Wizara imefanya mabadiliko ya viwango vya ada za matumizi mbalimbali ya maji vilivyokuwa vinatumika kuanzia 2002. Kiwango cha tozo cha Sh10 kwa kila lita ya maji kilitangazwa na kuanza kutumika kuanzia mwaka wa fedha 2014/2015.

Profesa Mbarawa alisema hatua hiyo ilifikiwa baada ya ada za awali kuwa ndogo ikilinganishwa na gharama halisi za usimamizi wa rasilimali maji.

Waziri huyo ameongeza kuwa tangu kipindi hicho, baadhi ya viwanda vimeshindwa kutekeleza agizo hilo, licha ya juhudi zinazofanywa na Bodi za Maji za Mabonde za kuhamasisha ulipaji ada hizo.

“Hivyo lengo la kikao chetu ni kuwashirikisha wadau wetu hatua hizo za wizara ili muweze kushirikiana nasi katika kazi hii muhimu ya utunzaji wa rasilimali za maji itakayotuletea manufaa ya kiuchumi yatokanayo na uzalishaji wa viwandani,”

Kwa upande wake, Ofisa wa Maji Bonde la Wami/Ruvu, Saimon Ngonyani amesema kuwa lengo la mkutano huo ni kuzungumza na wadau hao wanaozalisha maji ya chupa ambao wanapaswa kulipa Sh10 kila lita. Alisema kwa wazalishaji wa maji ya chupa ni wanne tu ndo hulipa tozo hiyo huku wengine wakidai hailipiki.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Historia ya marehemu Isaac Nyagabona Muyenjwa Gamba

HISTORIA YA MAREHEMU ISAAC NYAGABONA MUYENJWA GAMBA. Ratiba Kwa Ufupi Jumatatu Alfajiri – Kupokea Mwili Airport …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *