Home / Habari Za Kitaifa / JPM ATEUA MA-DED WAPYA 41, AHAMISHA WENGINE

JPM ATEUA MA-DED WAPYA 41, AHAMISHA WENGINE

RAIS John Magufuli amefanya uteuzi wa Mkuu wa Wilaya mmoja, Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji 41, na amewahamisha vituo vya kazi Mkuu wa Wilaya mmoja na Wakurugenzi wa Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji 19. Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Ikulu Dar es Salaam jana, ilieleza kuwa Rais Magufuli amemteua Senyi Ngaga kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mkoa wa Mwanza.

Ngaga amechukua nafasi ya Mhandisi Mtemi Simeon ambaye amehamishwa kituo cha kazi na kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chato mkoani Geita, baada ya Mkuu wa Wilaya ya Geita aliyeteuliwa hivi karibuni, Kanali Patrick Songea kwenda kwenye mafunzo ya kijeshi nje ya nchi. Taarifa hiyo ilieleza kuwa Rais Magufuli amefanya uteuzi na uhamisho wa Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji, kutokana na baadhi ya wakurugenzi waliokuwa katika nafasi hizo kustaafu, kupangiwa kazi nyingine, kuhamishwa na wengine kuondolewa katika nafasi za ukurugenzi kama ifuatavyo:

Mkoa wa Arusha

•Jiji la Arusha – Dk. Maulid Madeni. •Halmashauri ya Wilaya ya Meru – Emanuel Mkongo.

Mkoa wa Dar es Salaam

Manispaa ya Temeke – Lusubilo Mwakabibi (Amehamishiwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko Mkoani Kigoma). •Manispaa ya Ubungo – Beatrice Kwai (Amehamishiwa kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara). •Manispaa ya Ilala – Jumanne Kiango Shauri (Amehamishiwa kutoka Halmashauri ya Mji wa Korogwe). •Manispaa ya Kigamboni – Ng’wilabuzu Ludigija (Amehamishiwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa).

Mkoa wa Dodoma

•Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa – Mustafa Yusuph. •Halmashauri ya Mji wa Kondoa – Msoleni Dakawa. •Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa – Paul Sweya. •Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa – Dk. Omary Nkullo.

Mkoa wa Geita

•Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale – Mariam Chaurembo. •Halmashauri ya Wilaya ya Chato – Eliud Mwaiteleke (Amehamishiwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi).

Mkoa wa Iringa

•Halmashauri ya Manispaa ya Iringa – Hamid Njovu (amehamishiwa kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga).

Mkoa wa Kagera

•Halmashauri ya Wilaya ya Misenyi – Innocent Mukandala. •Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba – Limbe Maurice (amehamishiwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Misenyi). •Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba – Solomon Kimilike.

Mkoa wa Katavi

•Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo – Ramadhan Mohamed.

Mkoa wa Kigoma

•Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma – Mwailwa Pangani (Amehamishiwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo). •Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko – Masumbuko Magang’hila. •Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma – Upendo Mangali.

Mkoa wa Kilimanjaro

•Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga – Zefrin Lubuva. •Halmashauri ya Wilaya ya Moshi – Tatu Kikwete (Amehamishiwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha).

Mkoa wa Lindi

•Halmashauri ya Wilaya ya Liwale – Nassib Mmbaga (Amehamishiwa kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Temeke). •Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa – Renatus Mchau.

Mkoa wa Mara

•Halmashauri ya Wilaya ya Musoma – Kayombo John (Amehamishiwa kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo). •Halmashauri ya Wilaya ya Butiama – Magori Alphonce.

Mkoa wa Mbeya

•Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya – Stephan Katemba (Amehamishiwa kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni). •Halmashauri ya Jiji la Mbeya – James Kasusura. •Halmashauri ya Wilaya ya Kyela – Lucy Mganga.

Mkoa wa Morogoro

•Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero – Stephano Kaliwa. •Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro – Kayombe Lyoba. •Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi – Mussa Mnyeti. •Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa – Asajile Mwambambale.

Mkoa wa Mtwara

•Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara – Kanali Emmanuel Mwaigobeko.

Mkoa wa Mwanza

•Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi – Kisena Mabuba •Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe – Ester Chaula.

Mkoa wa Njombe

•Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe – Edes Lukoa (Amehamishiwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze). •Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa – Sunday George.

Mkoa wa Pwani

•Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze – Amina Kiwanuka (Amehamishiwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe). •Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha – Butamo Ndalahwa (Amehamishiwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Moshi).

Mkoa wa Rukwa

•Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi – Engelus Kamugisha. •Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo – Msongela Palela (Amehamishiwa kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala). •Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga – Jacob Mtalitinya (Amehamishiwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Nzega).

Mkoa wa Ruvuma

•Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga – Juma Mnwele. •Halmashauri ya Mji wa Mbinga – Grace Quintine. •Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo – Evans Nachimbinya. •Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru – Gasper Balyomi.

Mkoa wa Shinyanga

•Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga – Hoja Mahiba.

Mkoa wa Simiyu

•Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi – James Mtembelea.

Mkoa wa Singida

•Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi – Justice Lawrence

Mkoa wa Songwe

•Halmashauri ya Wilaya ya Tunduma – Mussa Natty. •Halmashauri ya Wilaya ya Songwe – Fauzia Hamidu. •Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi – Kazimbaya Makwega (Amehamishiwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto).

Mkoa wa Tabora

•Halmashauri ya Wilaya ya Nzega – Sekiete Yahaya. •Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge – Martha Luleka.

Mkoa wa Tanga

•Halmashauri ya Mji wa Korogwe – Nicodemus Bee. •Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi – Gracia Makota. •Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli – George Haule. •Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe –Kwame Daftari. •Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto – Ikupa Mwasyoge.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Historia ya marehemu Isaac Nyagabona Muyenjwa Gamba

HISTORIA YA MAREHEMU ISAAC NYAGABONA MUYENJWA GAMBA. Ratiba Kwa Ufupi Jumatatu Alfajiri – Kupokea Mwili Airport …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *