Home / Habari za Kimataifa / Watu 40 wameuawa katika mapigano ya jamii mbili tofauti mashariki mwa Ethiopia

Watu 40 wameuawa katika mapigano ya jamii mbili tofauti mashariki mwa Ethiopia


Mapigano ya jamii za Ethiopia na Somalia

Kufuatia mauaji ya watu 40 katika eneo la Negeri Lencho mashariki mwa Ethiopia,msemaji wa jimbo la jamii ya watu wa Oromia amesema waliouawa ni wa watu wa Oromo pekee.

Polisi wanasema katika tukio jingine wakulima wawili wa jamii ya Tigrayan walipigwa mawe hadi kufa ndani ya eneo la Oromia.

Takriban watu 40 wameuawa katika jimbo la Oromia mashariki mwa Ethiopia na watu wanaodaiwa kuwa kikosi kijulikanacho kama Liyu kutoka nchini Somalia.Uongozi wa maeneo hayo umeiambia BBC

Zaidi ya watu 40 walijeruhiwa wakiwemo watoto wanawake na mzee mmoja asiyeona ni miongoni mwa waliouawa.

Mmoja wa walionusurika katika shambulio hilo baada ya kudhaniwa kuwa tayari alikuwa amekufa,ameelezea kwamba uvamizi huo ulifanyika usiku.

Kumekuwa na mfululizo wa mauaji ya watu kadhaa katika mpaka wa Somali na Oromia na Zaidi ya watu milioni moja wameyakimbia makazi yao.

Vikosi vya serikali vimeimarisha ulinzi ili kukabilina na hali hiyo ambayo inaonekana kuwa ni m,achafuko ya kihistoria katika maeneo hayo.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mohamed Bin Salman

CIA ‘yamlaumu mwanamfalme wa Saudia ‘

Shirika la ujasusi la Marekani(CIA) linaamini kuwa Mwanamfalme Mohammed bin Salman wa Saudi Arabia ndiye …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *