Aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya uongozi ya Chama cha upinzani (CUF) Julius Mtatiro ,kuhamia CCM

Maswali mengi yamezuka mara baada ya aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya uongozi ya Chama cha Wananchi (CUF) Julius Mtatiro ,kujivua uanachama wake na kuhamia chama tawala cha CCM.

Mtatiro ni mwanasiasa ambaye pia ni mchambuzi wa siasa na amekuwa akiandika makala nyingi kuikosoa serikali lakini sasa amehamia huko ambako amekuwa akikukosoa kwa muda mrefu.

“Nimejiridhisha kwa hitaji la nafsi yangu kujiunga na Chama cha Mapinduzi CCM” Julius Mtatiro aliyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari siku ya jumamosi,Agosti 11.

Mkurugenzi wa habari wa chama cha CUF,Abdul Kambaya amesema zaidi ya asilimia 70 ya migogoro ya chama hicho imesababishwa na Mtatiro.

Chama hicho ambacho kimegawanyika katika pande mbili,kuna wale ambao ni wafuasi wa Profesa Ibrahim Lipumba na wale ambao wako chini ya Maalim Seif.

Awali chanzo cha migogoro ya ndani ya chama cha CUF ilidaiwa kuwa ni Profesa Lipumba kutangaza kutengua barua yake ya kujiuzulu nafasi ya uenyekiti aliyoiandika Agosti 2015, wakati wa kuelekea kwenye Uchaguzi mkuu.

Lakini kwa sasa mgawanyiko wa chama hicho umedaiwa kusababishwa na Julius Mtatiro kutokana na tabia zake za kibabe za kutotaka kusikiliza watu wengine.

Inakumbukwa kwamba mwanzoni mwa mwezi Julai,Mtatiro alikamatwa na polisi kutokana na ujumbe alioandika katika mtandao wa kijamii unaomkejeli rais John Magufuli kwa kusema kuwa ‘rais kitu gani?’

Aidha kujiengua kwa mwanasiasa huyo kumepelekea baadhi ya watumiaji wa mtandao wa kijamii kuanzisha kampeni za kuonesha kupinga au kukasirishwa na uamuzi wake kwa kuwataka watu waache kumfuatila kwenye mitandao ya kijamii kutokana na uamuzi wake kuonekana kuwa wa kisaliti.

Katika mtandao wa twitter wameanzisha #unfollowmtatiro na #blockmtatiro

 

Evarist Chahali

@Chahali

I just published “ : Msaliti Huyu Atapata Tabu Sana” https://medium.com/p/blockmtatiro-unfollowmtatiro-msaliti-huyu-atapata-tabu-sana-7b6c4a875c83 

#BlockMtatiro #UnfollowMtatiro: Msaliti Huyu Atapata Tabu Sana

Moja ya dhamira kuu za Magufuli ni kuua upinzani. Na hilo lilikuwa moja ya mambo ambayo yalitupa wasiwasi baadhi yetu tulioshiriki kumnadi…

medium.com

Lakini vilevile Mtatiro alikuwa ni kiongozi wa upinzani ambaye alikuwa anawabeza wanasiasa wengine kuhamia CCM lakini sasa yeye ndiye ameamua kuhamia CCM.

Pamoja na kwamba Julius Mtatiro alifahamika kuwa mwanachama wa CUF,ila mwezi julai mwaka huu jumuiya ya vijana za CUF(JuviCUF) ilimtaka Mtatiro kukaa mbali na chama hicho na kuacha tabia ya kuwashambulia viongozi wa juu wa chama cha CUF kupitia mitandao ya kijamii kwa kuwa wao hawamtambui kuwa mwanachama wa chama hicho na aache tabia ya kupotosha umma.

Hatimaye sasa kile ambacho chama cha vijana CUF walichokuwa wanakihofia kuwa mwanasiasa huyo sio mwenzao kimeweza kudhihirika wazi.

Mtatiro aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya uongozi ya CUF alitangaza kuhamia CCM siku ya jumamosi.

 

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mohamed Bin Salman

CIA ‘yamlaumu mwanamfalme wa Saudia ‘

Shirika la ujasusi la Marekani(CIA) linaamini kuwa Mwanamfalme Mohammed bin Salman wa Saudi Arabia ndiye …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *