Home / Habari za Kimataifa / DSTV, AZAM na ZUKU zatakiwa kuonyesha bure vipindi vya stesheni za Tanzania

DSTV, AZAM na ZUKU zatakiwa kuonyesha bure vipindi vya stesheni za Tanzania


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini Tanzania ,Dr.Harrison Mwanyembe

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini Tanzania ,Dr.Harrison Mwakyembe, amezitaka kampuni za vin’gamuzi vya DSTV, AZAM na ZUKU kufuata sheria kwa sababu Watanzania wana haki ya kupata habari bila kulipishwa.

Waziri huyo ameitaka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) izipe utaratibu kampuni hizo namna ambavyo zinaweza kurusha chaneli za ndani bure kama wamevutiwa na soko hilo.

Tanzania ilipoingia katika mfumo wa digitali kumekuwa na mfumo wa kulipia na hapo mwanzoni Tv zote zilikubaliana na zilipewa masharti kwa mfano mtazamaji anapata gharama mwanzoni tu anaponunua king’amuzi .

Wamiliki wa vin’gamuzi hivyo vya DSTV ,AZAM na ZUKU wote makao makuu yao yako nje ya nchi na maudhui yao ni ya kimataifa hivyo hata gharama za ulipaji wao leseni ni tofauti lakini ikija kwenye suala la matangazo ya ndani utaratibu upo pia na wanapaswa kuufuata.

“Kama hawa wenzetu wana hamu sana na soko hili la ndani waende TCRA wapewe utaratibu wa namna ya kuupata,” amesema Mwakyembe.

Waziri Mwakyembe alisisitiza kuwa ni haki ya Mtanzania kuweza kuhabarishwa kwa sababu chanzo cha mapato sio watazamani bali ni matangazo ndio maana hizi chaneli za umma wanatakiwa walipwe na maudhuhi yake ni ya ndani ya nchi.

Kuna mfumo wa kulipia lakini TBC, Star TV, ITV, Channel Ten na EATV ni lazima zirushwe bila malipo yoyote .

Dk. Mwakyembe pia amesisitiza kuwa serikali haijafuta leseni za visimbuzi/Ving’amuzi vya Azam, Zuku na DSTV Multichoice Tanzania bali wanawataka kuondoa chaneli ambazo zinatakiwa kurushwa bure kulingana na matakwa ya mikataba yao.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mohamed Bin Salman

CIA ‘yamlaumu mwanamfalme wa Saudia ‘

Shirika la ujasusi la Marekani(CIA) linaamini kuwa Mwanamfalme Mohammed bin Salman wa Saudi Arabia ndiye …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *