Home / Michezo / Petr Cech: Kipa wa Arsenal aishutumu Bayer Leverkusen kwa kumcheka kwenye Twitter

Petr Cech: Kipa wa Arsenal aishutumu Bayer Leverkusen kwa kumcheka kwenye Twitter

Mlinda lango wa Arsenal Petr Cech amewaeleza Bayer Leverkusen kuwa “wa kusikitisha” baada ya klabu hiyo ya Ujerumani kuonekana kumcheka kwenye mtandao wa kijamii wa twitter.

Cech nusura ajifunge alipokuwa anajaribu kudhibiti mpira wa kurejeshwa nyuma na mchezaji mwenzake Jumamosi.

Arsenal walilazwa 2-0 na mabingwa watetezi Manchester United nyumbani kwao Emirates.

Alichezeshwa langoni badala ya kipa mpya wa Arsenal Bernd Leno aliyenunuliwa £19m dirisha la kuhama wachezaji lililofungwa wiki iliyopita kutoka Leverkusen.

Klabu hiyo ya Bundesliga iliandika ujumbe kwenye Twitter kuhusu tukio hilo kwamba “huenda tunamfahamu jamaa fulani…” na kisha kuongeza video fupi ya kipa wao wa zamani.

Cech, aliyezungumza baada ya mechi hiyo alisema anajiamini katika uwezo wake wa kuisaidia timu kujijenga mchezoni kuanzia kwenye safu ya mashambulizi.

Aliandika kwenye Twitter Jumatatu usiku: “Katika Arsenal tuna maadili ya pamoja ambayo ni muhimu sana na ambayo hutufanya sio tu klabu kubwa ya soka,” aliandika. “Uchezaji na kushindana kwa haki, utaalamu na maadili mema ya uchezaji ni mambo ambayo huwa unawafunza wachezaji chipukizi na inasikitisha kuona kwamba kuna klabu nyingine hazifuati maadili haya.”

Leverkusen kisha walimjibu Cech na kusema kwamba ujumbe wao wa kwanza kwenye Twitter ulikuwa “utani” na wakamsifu kwa uchezaji wake siku hiyo.

“Hujambo Petr. Yamkini utani wetu kwamba tulitaka kumuona Leno, mchezaji wetu wa zamani, akichezeshwa umepokelewa vibaya kuliko tulivyotarajia. Ulikuwa ni mzaha tu. Sote tunaamini katika maadili uliyoyataja na tunakutakia wewe na klabu yako kubwa kila la heri. Ulifanya vyema kuokoa mpira ulipobaki wewe ukikabiliana na Aguero langoni.”

Cech alifanywa nahodha mechi ya kwanza ya Arsenal msimu huu

Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Ian Wright anasema alifikiria cech alionekana kuwa na wasiwasi kila aliporejeshewa mpira na wachezaji wenzake.

“Inakubidi ucheke bila kutaka, mashabiki walikuwa wanasema kwa sauti ‘uondoe tafadhali.’ Pengine kuanza kucheza hivyo dhidi ya moja ya timu bora zaidi Ulaya halikuwa wazo njema.”

Chris Sutton amesema anafikiri Arsenal walikuwa na uamuzi mgumu wa kufanya, kwamba walitumia £20m kumnunua kipa kisha wamuweke benchi.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Nyota wa Afrika wamkumbuka mmiliki wa Leicester City Vichai Srivaddhanaprabha

Riyad Mahrez (kushoto) ni mmoja ya walitoa heshima zao kwa Vichai Srivaddhanaprabha Wachezaji wa Kiafrika …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *