Home / Habari za Kimataifa / Ni kwa nini China inataka kuubomoa msikiti huu mpya

Ni kwa nini China inataka kuubomoa msikiti huu mpya

China ina mipango ya kudhibiti jinsi madhehebu ya dini huendesha shughuli zao, lakini mipango ya kuubomoa msikiti kwenye mji ambao umekuwa ukitii sheria huenda ikazua madhara, kwa mujibu wa msomi mwenye makao yake nchini Marekani David R Stroup.

Asubuhi moja mapema Februari mwaka 2016, nilisimama nje ya msikiti huko Weizhou, ambao ni mji mdogo wenye waislamu wengi eneo la Ningxia Hui.

Kando yangu karibu wanaume 150 wengi wakiwa na mavazi meupe wakiwa na ndevu, walitembea kwa haraka kwenda kwenye vyoo vya msikiti kujiandaa kwa maombi ya kwanza ya siku – Salat al-fajir.

Kutoka mbali vipaza sauti vya misikiti mingine vilisikika vikitangaza maombi. Huku sauti hizo zikisikika kote mjini, wanaume walikusanyika na kuanza kuomba kuanza siku nyingine mpya katika eneo hilo lenye wakazi wengi waumini wa kiislamu.

Miaka miwili baadaye mji huo mdogo wa Weizhou umejipata ndani ya mzozo unaokua kati ya serikali na waislamu ambao wanapinga mpango wa kuubomoa msikiti ambao ujenzi wake umekamilika hivi majuzi.

Serikali ya masnispaa ilisema ilikuwa na haki ya kuubomoa msikiti huo kutokana na sababu kuwa msikiti huo, haakupata vibali sahihi vya ujenzi hali ambayo imeufanya uwe mjengo haramu. Kujibu, wakaazi wengi wa Hui ambao ni waislamu waliuzingira kuzuia kubomolewa kwake.

Mzozo huo umekuwa mbaya, Serikali sasa imeahidi kuwa haitaubomoa msikiti wote lakini inashikilia msimamo kuwa itafanyia marekebisho masuala fulani.

Lakni kufanya hivyo kutasabaisha kubomolewa kwa ishara ya mafanikio ya mji wa Weizhou.

Idadi ya watu wa Weizhou ni zaidi ya asilimia 90, wengi wa jamii ya Hui. Wakiwa mara nyingi wanatajwa na vyombo vya habari kama Waislamu wa China, Hui ni waislamu waliowasili China wakati wa utawala wa Tang karne ya nane.

Licha ya historia ya kuwepo mizozo na jamii inayotawala ya Qing karne ya 18 na 19, Hui wamekuja kutajwa na wengi nchini China kama jamii ndogo ya kisasa, kulingana na vile mtu mmoja niliyemhoji kwenye kwenye mji wa Yinchuan aliniambia.

Wakati wa muda wangu nikifanya utafiti kwenye mji, wakazi waliniambia kuwa watu wengi walivaa hijab na kofia nyeupe za kitamadunia. Karibu kila mtu alienda msikitini kuomba kila siku. Hakuna duka lililouza pombe kijijni.

Msikiti ambao wakati huo ndio ulikuwa unajengwa, ulikuwa kitua cha jamii kujivunia. Baada ya kukamilika utakuwa mkubwa zaidi huko Ningxia uliojengwa kwa kile wenyeji wanasema ni mfumo wa kiarabu.

Utakuwa mkubwa wa kuitosha jamii nzima inapokusanyika kwa maombi ya Ijumaa. Chini ya mwaka mmoja tangu ukamilike msikiti huo umejipata kwenye mzozo.

Moja ya mifano mikuu ya athari za kampeni ni kutoka eneo la kaskazini magharibi la Xinjian wanamoishi jamii ya Uighur.

Ripoti ya hivi majuzi ya jopo la Umoja wa Mataifa inadai kuwa karibu watu milioni moja wa jamii ya Uighur wamezuiwa kwenye kambi za mafunzo baada ya kulaumiwa na serikali wana itikadi kali, kutokana na masuala madogo kama kuvaa hijab, kusafiri ng’ambo au kusambaza maandiko kutoka kwa Qur’an.

Hata baada ya wito kutoka nchi za kigeni za kuitaka China kusitisha oparesheni hiyo, serikali imedumisha kuwa wakosoaji wa kigeni hawaelewi hali ilivyo.

Licha ya oparesheni kuwa kali huko Xinjian, sehemu zingine za jamii za Hui hasa zile zilizo Ningxia zimehisi athari zilizopo.

Sawa na sehemu zingine za magharibi mwa China maendeleo ya mji huo yalibaki nyuma na yale ya pwani ya kusini. Miaka ya tisini Weizhou ulikumbwa na umaskini mkubwa na janga la matumizi ya heroine.

Kampeni kubwa ya maendelea ya magharibi ilimwaga pesa nyingi miaka ya 2000 kwenye miji kama Weizhou na kwa msaada huu wa kiuchumi watu wa mji huu mdogo wa Hui walijikwamua kutoka umaskini na kujiunga na tamaduni za kiislamu.

Watu wakaanza kufanya biashara na wakawa wenye maendeleo. Jamii hii ilifungua shule kwa watoto maskini kujifunza na kusoma Koran.

Watu wakaanza kuomba kila wakati. Mtu mmoja nilizungamza naye aliniambia: “Watu wana maisha ya kawaida, Hakuna majengo marefu, lakini wenyeji ni watu wenye maendeleo mengi. Maisha ni mazuri.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mohamed Bin Salman

CIA ‘yamlaumu mwanamfalme wa Saudia ‘

Shirika la ujasusi la Marekani(CIA) linaamini kuwa Mwanamfalme Mohammed bin Salman wa Saudi Arabia ndiye …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *