Home / Habari Za Kitaifa / Mwenyekiti Halmashauri Mbaroni Kwa Kuhamisha Bila Kulipa

Mwenyekiti Halmashauri Mbaroni Kwa Kuhamisha Bila Kulipa

Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Brigedia Nicodemas Mwangela amempeleka mahabusu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, Elick Ambakisye kwa kuwahamisha wafanyakazi wa vituo vya afya kabla ya kuwalipa mafao yao.

Kwa kufanya maamuzi hayo anadaiwa kukiuka agizo la Rais John Magufuli kwa kuwataka watumishi wasihamishwe bila kupewa mafao yao.

Ilidaiwa kwamba mwenyekiti huyo ameagizwa kuhamishwa kwa watumishi wa afya 106 kutoka hospitali ya mkoa kuhamia vituo vingine vya afya ndani ya wilaya hiyo.

Agosti 24 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi kwenye kikao cha baraza la madiwani aliwataka watumishi wa afya 106 kutoka hospitali ya Viwawa iliyopandishwa hadhi kuwa hospitali ya mkoa kuhamia katika hospitali ya Nanyara iliyopandishwa kuwa hospitali ya wilaya ya Mbozi.

Katibu Tawala Mkoa wa Songwe akizungumza juzi kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Songwe, Brigedia Mwangela ambaye yupo Dodoma kikazi alisema kuwa mwenyekiti wa halmashauri hiyo ameitwa na jeshi la polisi ili kuhojiwa kuhusu uhalali wa kauli yake aliyoitoa kuhusu watumishi wa afya kuhamia vituo vya afya bila kupewa stahiki zao kinyume na agizo la Rais.

Hata hivyo madiwani wamekuja juu na kudai kuwa kwenye maofisa wahusika walikuwepo kwenye baraza hilo na hawakutoa ushauri baada ya mwenyekiti kutoa maelekezo ya kuhamisha wafanyakazi kuhudumia maeneo mengine.

Allan Mgulla diwani wa kata ya Itaka alisema maelezo yote aliyotoa siku ya Baraza mwenyekiti wao kuwa viongozi wote na watumishi wa umma walikuwepo na hawakutoa ushauri wala maelekezo yoyote kuhusu tamko la kuwaomba watumishi wa afya kuhamia kituo cha afya cha Nanyara ambacho kilipitishwa na kikao kuwa hospitali ya wilaya ya Mbozi.

Mgulla aliwataja baadhi ya viongozi ambao walikuwepo katika kikao hicho cha baraza la madiwani cha Agosti 24 kuwa ni pamoja na katibu tawala mkoa, mkuu wa wilaya, mkurugenzi wa wilaya ya Mbozi na watumishi wengine wa halmashauri akiwemo kaimu mganga mkuu mkoa na mwanasheria wa serikali. Naye Richard Kibona Diwani wa Ilolo alisema: ‘

’Watalaamu wote walikuwepo siku ya baraza kama mwenyekiti alikosea basi wangetushauri kwenye kile kikao cha baraza kwa kuwa ndio kazi yao kwetu sisi, tunashangaa mwenyekiti kukamatwa hii leo kwa kauli ya kuokoa maisha ya watu”.

Rais John Magufuli ametoa agizo kuwa watumishi wote nchini kutohama katika vituo vyao vya kazi pasipokupewa stahiki zao muhimu baada ya kubadilishiwa vituo vya kazi .

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Historia ya marehemu Isaac Nyagabona Muyenjwa Gamba

HISTORIA YA MAREHEMU ISAAC NYAGABONA MUYENJWA GAMBA. Ratiba Kwa Ufupi Jumatatu Alfajiri – Kupokea Mwili Airport …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *