Home / Habari za Kimataifa / Waombolezaji Ghana waghadhabishwa kwa kufunikwa jeneza la Kofi Annan

Waombolezaji Ghana waghadhabishwa kwa kufunikwa jeneza la Kofi Annan

Raia Ghana wanatoa heshima zao za mwisho kwa katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa mataifa Kofi Annan kabla ya maziko Alhamisi

Raia Ghana wanatoa heshima zao za mwisho kwa katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa mataifa Kofi Annan

Mwili wake Annan umelazwa katika ukumbi wa mikutano ya kimataifa Accra akitarajiwa kuzikwa Alhamisi

Vyombo vya habari Ghana vinaeleza kwamba baadhi ya waombolezaji hawakuridhishwa na hatua ya jeneza la Annan kufinikwa na kuwazuia waombolezaji kumuona kwa mara ya mwisho kiongozi huyo wa zamani.

Mjane wa aliyekuwa rais wa kwanza afrika kusini Nelson Mandela – Bi Graca Machel na Gro Harlem Brundtland ambaye aliwahi kuwa waziri mkuu nchini Norway ni miongoni mwa wanaohudhuria mazishi ya Annan

Sehemu ya shughuli zinajumuisha maafisa kutoa heshima zao kwa jamaa na familia ya Annan.

Hizi ndio baadhi ya picha za karibu zilizopigwa na waandishi wa BBC Ayo Bello na Mayeni Jones zinazoonyesha msafara kutoka jimbo alikozaliwa Annan- Akwamu – ukiwasili katika jumba hilo la mikutano ya kimataifa mjini Accra.

Annan, ni kiongozi wa pili wa Afrika kuishikilia nafasi ya katibu mkuu wa Umoja wa mataifa. Alifariki mwezi Agosti akiwa na miaka 80.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mohamed Bin Salman

CIA ‘yamlaumu mwanamfalme wa Saudia ‘

Shirika la ujasusi la Marekani(CIA) linaamini kuwa Mwanamfalme Mohammed bin Salman wa Saudi Arabia ndiye …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *