Home / Habari za Kimataifa / Tume ya Ulaya yalenga kubuni ajira milioni 10 barani Afrika

Tume ya Ulaya yalenga kubuni ajira milioni 10 barani Afrika


Jean-Claude Juncker

Rais wa tume ya Ulaya Jean-Claude Juncker amependekeza kuwepo kwa muungano mpya na Afrika, kuboresha uhusiano wa kiuchumi na pia kuongeza uwekezaji na ajira.

Kwenye hotuba yake ya kila mwaka Bw Juncker alisema mpango huo utasaidia kubuniwa mamilioni ya ajira barani Afrika katika kipindi cha miaka mitano inayokuja.

Maoni ya Bw Juncker yanahusu kile anachokiita biashara huru kati ya mabara. “Suala hapa ni kuboresha mikatati iliyopo sasa ambayo inazipa karibu nchi zore za Afrika uwezo wa kufikia masoko ya Ulaya bila kodi.”

Pendekezo hilo pia linawapa fursa zaidi watu kutoka afrika kuongeza maarifa kwa mfano kwa kusomea viuo vikuu vya Ulaya.

Walinzi wa mipaka na pwani za Ulaya

EU inapendekeza Jumla ya euro bilioni 40 katika kipindi cha miaka saba hadi mwaka 2021. “EU inataka kupanua uhusiano wake na Afrika ambayo ni sehemu muhimu sana duniani.”

Pia Juncker alitangaza mipango ya EU kutuma walinzi wa mipaka 10,000 kukabiliana na uhamiaji haramu ifikapo mwaka 2020.

Hii ndiyo hotuba ya mwisho ya Bw Juncker kama rais wa Jumuiya ya Ulaya.

Mashirika ya Frontex na lile na ulinzi wa mipaka na pwani za Ulaya kwa sasa yamewaajiri watu 1,600

Mambo yaliyozungumziwa na Juncker…

Kuhusu usalama

Bw Jucker alisema EU inahitaji kuwa salama kutoka kwa vitisho vingi vinavyoikumbwa.

“Ni Ulaya dhabiti tu na yenye nguvu inayoweza kuwalinda watu wake kutokana vitisho vya nje na vya ndani – kutokana wa ugaidi na mabadiliko ya hali ya hewa.”

Kuhusu uhamiaji

Mashirika ya Frontex na lile na ulinzi wa mipaka na pwani la Ulaya kwa sasa yamewajiri walinzi 1,600 kutoka Ulaya, kwa hivyo idadi mpya inayotajwa na Juncker ni ongezeko kubwa.

Bw Juncker zaidi alipendekeza kubuniwa shirika linahusika na kutoa hifadhi barani Ulaya amabalo litatoa msaada kwa nchi zinazowapa hifadhi watafuata hifadhi.

Alisisitiza hitaji la kuwepo njia halali za kuingia Ulaya. “tunahitaji wahamiaji wenye ujuzi,” alisema.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mohamed Bin Salman

CIA ‘yamlaumu mwanamfalme wa Saudia ‘

Shirika la ujasusi la Marekani(CIA) linaamini kuwa Mwanamfalme Mohammed bin Salman wa Saudi Arabia ndiye …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *