Home / Habari za Kimataifa / Watu 50 Wapoteza Maisha Congo Katika Ajali

Watu 50 Wapoteza Maisha Congo Katika Ajali

ajali congo

Takriban watu 50 wameuawa baada ya trela ya kusafirisha mafuta kugongana na gari ndogo katika barabara kuu magharibi kwa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo.

Ajali hiyo ilitokea karibu na mji wa Kisantu, kati ya mji mkuu Kinshasa na bandari ya Matadi.

Watu 100 walipata majeraha mabaya ya moto kwa mujibu wa Atou Matabuana, gavana wa mkono wa wa Kongo Central.

“Moto ulisambaa kwa haraka na kuteketeza nyumba zilizokuwa karibu,”hii ni kwa mujibu wa redio ya Umoja wa Mataifa ya Okapi.

Barabara kati kati mwa nchi zimetelekezwa kwa miaka mingi kutokana na vita.

Mwaka 2012 watu 220 waliuawa wakati trela ya mafuta ilipinduka na kuteketeza vijiji kadhaa.

Mmoja wa wale walioshuhudia aliiambia AFP kuwa aliona milii 53.

Daktari kwenye hospitali moja anayewatibu majeruhi alisema hakujakuwa na muda wa kuwapa matibabu waathiriwa.

‘Tuanajaribu kuwasaidia lakini kuna wale wanakufa,” Dr resor alisem.

Mji wa Kisantu uko umbali wa kilomita 120 kusini magharib mwa Kinshasa.

 

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mohamed Bin Salman

CIA ‘yamlaumu mwanamfalme wa Saudia ‘

Shirika la ujasusi la Marekani(CIA) linaamini kuwa Mwanamfalme Mohammed bin Salman wa Saudi Arabia ndiye …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *