Home / Habari Za Kitaifa / RADI YAUA MTOTO WA MCHUNGAJI

RADI YAUA MTOTO WA MCHUNGAJI

MTOTO wa Mchungaji wa Kanisa la Evangelic, Dorcas Andrew (5) amekufa baada ya radi kumjeruhi vibaya kifuani huku mama yake mzazi, Rhoda Mlela (36) akilazwa kwa matibabu katika Kituo cha Afya kata ya Sopa, wilaya ya Kalambo, mkoani Rukwa baada ya kupoteza fahamu.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa, George Kyando amethibitisha kutokea kwa tukio hilo juzi saa 11:00 jioni katika kijiji cha Sopa kilichopo katika wilaya ya Kalambo.

Akizungumza na gazeti hili, Mganga Mfawidhi wa kituo hicho cha afya, Severine Maembe alikiri kumpokea mtoto huyo kituoni hapo juzi jioni lakini alikuwa tayari amekufa.

“Jana(juzi) jioni mtoto huyo aliletwa kituoni hapa kwa matibabu baada ya kupigwa radi akiwa anacheza na watoto wenzake lakini nilipomwangalia alikuwa tayari amekufa, alikuwa amejeruhiwa vibaya sana kifuani,” alieleza.

Aliongeza kuwa mama mzazi wa mtoto huyo amelazwa katika kituo hicho kwa matibabu baada ya kupoteza fahamu muda mfupi baada ya kuelezwa kuwa binti yake amekufa baada ya kupigwa na radi.

Baadhi ya mashuhuda wanaeleza kuwa siku ya tukio Dorcas na mama yake walishuka kwenye gari kijijini hapo wakitokea mjini Sumbawanga ambapo mtoto huyo alipokewa na watoto wa rika lake na kuanza kucheza pamoja huku mama yake mzazi akielekea nyumbani.

“Watoto walikuwa sita pamoja na Dorcas wakicheza chini ya mti, ghafla ikapiga radi na kumjeruhi vibaya mtoto huyo huku wengine wakirushwa huku na kule lakini hakuna aliyejeruhiwa, wote ni wazima ila walipata mshtuko tu,” alieleza mtoa taarifa.

Mashuhuda hao ambao hawakuwa tayari majina yao kuandikwa gazetini kwa nyakati tofauti walidai kuwa mvua ilikuwa hainyeshi wakati radi ilipopiga kijijini hapo.

SOURCE HABARI LEO

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

CCM YASHINDA UBUNGE, UDIWANI KWA 100%

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimeshinda kwa asilimia 100 kwenye uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Buyungu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *