Home / Habari Za Kitaifa / PINDA AFIWA NA BABA YAKE MZAZI

PINDA AFIWA NA BABA YAKE MZAZI

BABA wa Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda, Xavery Mizengo Pinda (90) amefariki dunia katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, alikokuwa akitibiwa.

Tangazo lililotolewa jana na Mwandishi wa Waziri Mkuu, Irene Bwire, lilieleza kuwa Waziri Mkuu mstaafu, Pinda, anasikitika kutangaza kifo cha baba yake mzazi.

Kwa mujibu wa tangazo hilo, mzee Xavery Pinda alifariki jana saa 9:30 alasiri hospitalini hapo.

“Mizengo Peter Pinda, Waziri Mkuu mstaafu anasikitika kutangaza kifo cha baba yake mzazi, Mzee Xavery Mizengo Pinda (90), kilichotokea leo (jana) Tarehe 27 Novemba, 2016, saa 9:30 alasiri katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma,” lilieleza tangazo hilo.

Kutokana na kifo hicho, Pinda katika tangazo hilo aliwataarifu ndugu walioko katika kijiji cha Kibaoni, wilayani Mlele, mkoani Katavi, walioko nje, viongozi wa serikali na chama tawala na vyama vingine vya siasa kuhusu msiba huo.

Tangazo lilieleza kuwa taratibu za maziko zinafanyika nyumbani kwa Pinda, Zuzu, mkoani dodoma na taarifa zaidi zitatolewa baadaye.

SOURCE HABARILEO.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

CCM YASHINDA UBUNGE, UDIWANI KWA 100%

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimeshinda kwa asilimia 100 kwenye uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Buyungu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *