Home / Habari Za Kitaifa / MAJALIWA AFUTA MAADHIMISHO YA WALEMAVU KITAIFA

MAJALIWA AFUTA MAADHIMISHO YA WALEMAVU KITAIFA

MAADHIMISHO ya siku ya watu wenye ulemavu duniani, ambayo kitaifa yalitarajiwa kufanyika Desemba 3, mwaka huu Dar es Salaam, yameahirishwa na sasa kila mkoa utaadhimisha kivyake kupunguza gharama.

Akitoa tamko la kuahirishwa kwa maadhimisho hayo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), George Simbachawene, amesema maombi ya halmashauri za wilaya ni kuwasafirisha wanachama wa vyama vya watu wenye ulemavu ili wafanye maadhimisho hayo jijini Dar es Salaam.

Amesema maelekezo yaliyotolewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwa wakuu wa mikoa ni kwamba badala ya maadhimisho hayo ya kitaifa kukusanya watu wenye ulemavu wote kwenye mikoa kwenda Dar es Salaam wafanye katika mikoa yao.

“Nichukue nafasi hii kuwaagiza wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya na wakurugenzi kuhakikisha wanatoa ushirikiano wa kutosha wa vyama hivi ili viweze kufanikisha maadhimisho hayo,” alisema Simbachawene.

Amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, ahakikishe katika eneo walilopanga kufanya shughuli hiyo kwa kuwapa msaada utakaostahili.

Simbachawene amesema hali hiyo itasaidia kupunguza gharama badala ya wote wangesafirishwa kutoka mikoani na kwenda Dar es Salaam na sasa yafanyike kwenye mikoa na wilaya.

SOURCE HABARI LEO

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

CCM YASHINDA UBUNGE, UDIWANI KWA 100%

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimeshinda kwa asilimia 100 kwenye uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Buyungu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *