Home / Habari Za Kitaifa / ‘NYARAKA MUHIM U ZILIIBIWA KUTOKA BENKI YA EXIM’

‘NYARAKA MUHIM U ZILIIBIWA KUTOKA BENKI YA EXIM’

SHAHIDI wa 24 katika kesi ya wizi, kugushi na kutakatisha fedha zaidi ya Sh bilioni saba, inayowakabili waliokuwa wafanyakazi 13 wa Benki ya Exim tawi la Arusha, Inspekta John Mwakalenga (40) ameieleza Mahakama kuwa baadhi ya nyaraka muhimu za kesi hii ziliibwa katika benki hiyo.

Mwakalenga alirudia tena kutoa ushahidi wake juzi kwa mujibu wa sheria na kusema kuwa taarifa ya kuibwa kwa baadhi ya nyaraka hizo walipewa na uongozi wa benki hiyo, tawi la Arusha.

Shahidi huyo alisema hayo wakati akihojiwa na wakili wa upande wa utetezi, Adamu Jabir na kusema kuwa alikuwa miongoni mwa timu ya makachero wa upelelezi waliofanya upelelezi katika kesi hiyo na kuripoti kwa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoani Arusha (RCO).

Mwakalenga alisema uongozi wa Benki ya Exim ulieleza kwa maandishi kuwa baadhi ya nyaraka zilizotumika katika wizi huo ziliibwa na katika upelelezi wao waligundua kuwa fedha taslimu za kitanzania na dola, ziliibiwa katika benki hiyo kwa kutumia mfumo wa kibenki ujulikana kwa jina la CBS.

Alisema katika uchunguzi huo Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) ilipata hasara katika wizi huo na Benki ya Exim ndio walalamikaji katika kesi hiyo.

Shahidi huyo alisema baada ya kuambiwa hivyo, pamoja na wenzake waliamua kufanya uchunguzi kwa baadhi ya kampuni zilizokuwa zikilipa dola ili kupata huduma katika Hifadhi ya Ngorongoro na kupata baadhi ya ushahidi katika kesi hiyo.
SOURCE HABARI LEO

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

CCM YASHINDA UBUNGE, UDIWANI KWA 100%

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimeshinda kwa asilimia 100 kwenye uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Buyungu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *