Home / Michezo / OMOG: YANGA ITAJUTA KUMUONDOA PLUIJM

OMOG: YANGA ITAJUTA KUMUONDOA PLUIJM

Kocha mkuu wa Simba Joseph Omog, amesema kitendo cha Yanga kubadilisha kocha kimempa uhakika wa ubingwa msimu huu kwani awali alikuwa akimhofia sana Hans van der Pluijm.

Omog amesema, japo hamjui kocha mpya George Lwandamina, zaidi ya kusoma rekodi zake lakini Mzambia huyo hamtishi na anauhakika wataifunga Yanga kwenye mzunguko wa pili.

“Yanga wamefanya kosa kubwa kumbadili Van der Pluijm, kwasababu, ndiye kocha niliyekuwa namuhofia rekodi zake ndani ya Yanga hakuna kocha anayemfikia hata uchezaji wa timu ulikuwa wa hali ya juu, lakini ameondoka naweza kusema Simba ndiyo mabingwa wapya msimu huu,’amesema Omog.

Kocha huyo amesema hamdharau Lwandamina, lakini anaamini kocha huyo atabidi kusubiri sana ili kupata mafanikio aliyoyapata akiwa na Zesco United kutokana na utofauti wa mazingira ya alipotoka na alipo hivi sasa.

Amesema kama kocha mwenye deni la ubingwa kwenye klabu yake ya Simba amefurahia mabadiliko hayo kwasababu yamemrahisishia ugumu uliokuwa unamkabili kutokana na presha ya Yanga ambayo kwasasa wanatofautiana nao pointi mbili.

“Simwombei mabaya Lwandamina, lakini asitarajia kupata mafanikio katika msimu wake wa kwanza na mbaya zaidi ameikuta timu katikati ya msimu na ushindani ni mkubwa kila timu ikitaka pointi tatu,”amesema Omog.

Mcameroon huyo amekizungumzia kikosi chake na kusema kinaendelea vizuri na maandalizi yao na amepanga kuanza na mazoezi ya kurudisha nguvu kabla ya kuendelea na mambo mengine.

“Unajua walikuwa kwenye mapumziko kwaiyo nilazima tuanze na mazoezi ya nguvu ili kuuweka mwili sawa na baada ya hapo tutaendelea na mambo mengine kama mbinu na mifumo ya uchezaji,”amesema.

Kocha huyo pia amesema amefuraishwa na kazi nzuri iliyofanywa na uongozi wake wa kumleta nchini kipa Daniel Agyei, ambaye yupo nchini kwa ajili ya mazungumzo ya kuidakia timu yao kuanzia mzunguko wa pili.

Simba ilianza mazoezi ya kujiandaa na mzunguko wa pili tangu Jumatatu wiki iliyopita ikiwa chini ya kocha msaidizi Jackson Mayanja, akimshikia boss wake Omog ambaye alichelewa kutokana na kuuguliwa na Mama yake mzazi.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Willian anasema hakuna sababu ingemfanya kusalia Chelsea iwapo Antonio Conte angebakia

Willian alifunga magoli 13 na kutoa pasi 12za usaidizi katika mechi 55 za Chelsea msimu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *