Home / Michezo / Aliyetupiwa virago Simba aibuka mchezaji bora Rwanda

Aliyetupiwa virago Simba aibuka mchezaji bora Rwanda

Pierre Kwizera akikabidhiwa tuzo yake ya mchezaji bora wa mwaka ( Picha Hisani ya Ferwafa)

Pierre Kwizera ambaye kwa sasa anaichezea Rayon Sport ametangazwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Rwanda.

Kwizera aliwahi kuichezea Simba katika msimu wa 2014/15 kabla ya kutupiwa virago wakati wa dirisha dogo kwa madai ya kuchemsha.

Rayon Sports ilimsajili na msimu huu alifanya vizuri ikiwemo kufunga mabao saba na kuisaidia klabu hio kumaliza katika nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu ya Rwanda inayodhaminiwa na Azam Tv.

Pia alichangia klabu yake kubeba taji la Kombe la Amani nchini humo.

Katika tuzo hizo, Abdul aliwabwaga Muhadjiri Hakizimana wa Mukura Victory na mwenzake wa Rayon Sports, Savio Nshuti na kujinyakulia kitita cha faranga za Rwanda laki 5 sawa na shilingi milioni 1.4 za Tanzania.

Ulikuwa ni usiku mzuri kwa Rayon ambayo ilishinda tuzo nyingine, kocha wake Masudi Juma alizoa tuzo ya kocha bora mpya na kuwafunika Mtunisia Nizar Khanfir wa APR na Innocent Seninga wa Etincelles.

Rayon walizoa tuzo nyingine kupitia kwa Savio Nshuti Dominique ali aliyebaba tuzo ya mchezaji bora chipukizi.

Tuzo ya Kocha bora ilikwenda kwa Eric Nshimiyimana wa AS Kigali ambaye alimbwaga ally Bizimungu wa Bugesera na Okoko Godefroid wa Mukura Victory.

Tuzo ya mfungaji bora ilikwenda kwa Muhadjiri Hakizimana wa Mukura Victory na Dany Usengimana wa Polisi waliofunga mabao 16 kila mmoja.

Orodha Kamili ya washindi:

Wafungaji Bora
1. Hakizimana Muhadjiri (Mukura VS) -Mabao 16
2. Dany Usengimana (Police Fc)-Mabao 16

Mchezaji Bora wa mwaka: Kwizera Pierrot (Rayon Sports)

Mlinda mlango bora: Ndayishimiye Eric (Rayon Sport)

Kocha bora: Eric Nshimiyimana (AS Kigali)

kocha bora mpya: Masudi Djuma (Rayon Sport)

Mwamuzi Bora: Hakizimana Louis

Mwamuzi msaidizi bora: Niyonkuru Zephanie

Mchezaji chipukizi bora: Nshuti Savio Dominique (Rayon Sports)

Timu bora ya Msimu: Eric Ndayishimiye (Rayon Sport), Fitina Omborenga (SC Kiyovu), Imanishimwe Emmanuel (Rayon Sport), Munezero Fiston (Rayon Sport), Rwatubyaye Abdul (APR), Pierrot Kwizera (Rayon Sport), Ally Niyonzima (Mukura VS), Muhadjiri Hakizimana (Mukura VS), Savio Nshuti Dominique (Rayon Sport), Diarra Ismailla (Rayon Sport) na Iranzi Jean Claude (APR Fc)

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Willian anasema hakuna sababu ingemfanya kusalia Chelsea iwapo Antonio Conte angebakia

Willian alifunga magoli 13 na kutoa pasi 12za usaidizi katika mechi 55 za Chelsea msimu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *