Home / Habari Za Kitaifa / MSICHANA AONGOZA DARASA LA SABA KIMKOA

MSICHANA AONGOZA DARASA LA SABA KIMKOA

MWANAFUNZI wa kike kutoka Shule ya Msingi Ignatius, Manispaa ya Dodoma, Maria Segasii, amekuwa mshindi kimkoa katika mtihani wa darasa la saba uliofanyika Septemba mwaka huu kwa kupata alama 235, wakati katika matokeo ya mwaka 2015, mwanafunzi wa kwanza alipata alama 236 na alitoka shule ya msingi Mtejeta wilayani Mpwapwa.

Msichana wa kwanza kutoka shule za serikali ni Naima Mkusa anatoka shule ya msingi Mtejeta, Mpwapwa na alipata alama 219. Hayo yamo kwenye taarifa ya matokeo ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi 2016 na uchaguzi wa wanafunzi wa kidato cha kwanza 2017.

Mvulana wa kwanza kimkoa, Brian Assey anatoka shule ya msingi Ignatius kwa kupata alama 233 na katika ushindi wa jumla, ameshika nafasi ya pili.

Mwanafunzi wa kwanza kutoka shule za serikali ni Innocent Walazi anatoka shule ya msingi Pwaga katika halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa akiwa na alama 223 na ameshika nafasi ya 45 katika ushindi wa jumla.

Wanafunzi wasichana walioongoza kutoka shule za serikali ni Naina Mkusa, Mtejeta Mpwapwa; Mariam Mkiva, Chamwino, Dodoma Mjini; Fatuma Hassan, Nkulari, Chemba; Nuru Amos Mvumi, Chamwino; Sofia Ndeleka NDC- NARCO Kongwa; Imelda Raphael Ipagala Dodoma; Asha Iteu Nkurali, Chemba; Rahma Hemed na Johari Senyangwa wote kutoka NARCO- Kongwa na Martina Mwanitu wa Mnyakongo Kongwa.

Kata 10 zenye ufaulu wa kati ya daraja A hadi C, zimeongezwa na Chemchem (Kondoa Mjini) kwa ufaulu wa asilimia 97.65, tofauti na mwaka 2015 ilipopata asilimia 96. Kati ya kata hizo, tatu ni za manispaa ya Dodoma, mbili za Kondoa Mjini, tatu za halmashauri ya Kondoa, mbili za Chamwino na kata moja ya Kongwa.

Katika mtihani huo, kata ya mwisho kabisa ni Chunugulu (Chamwino) yenye ufaulu wa asilimia 14.75 ambayo mwaka 2015 ilikuwa na ufaulu wa asilimia 35 na kuwa nafasi ya 138, wakati mwaka 2015 kata ya mwisho ilikuwa Lufu ya Mpwapwa kwa kupata ufaulu wa asilimia nne. Shule 10 za kwanza za serikali ni NDC-NARCO (Kongwa), Madege, Kwadimu na Potea, Salare (Kondoa), Buigiri wasioona (Chamwino), Madisa, Sauna (Kondoa), Lupeta (Mpwapwa) na Chikopelo Bwawani (Bahi).

Kata 10 za mwisho za mwaka 2016 tanzo zinatoka Chamwino, tatu zipo Mpwapwa na mbili zinatoka Dodoma mjini.

Akizungumza wakati wa kikao cha wadau wa elimu juzi, Ofisa Elimu Mkoa wa Dodoma, Maria Lyimo alisema, wanafunzi 21,663 sawa na asilimia 99 ya waliofaulu pamoja na wa bweni 121 na wenye ulemavu 16, wanapendekezwa kuingia kidato cha kwanza 2017.
SOURCE HABARI LEO

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

CCM YASHINDA UBUNGE, UDIWANI KWA 100%

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimeshinda kwa asilimia 100 kwenye uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Buyungu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *