Home / Habari Za Kitaifa / RC- MUOMBENI RAIS MAGUFULI

RC- MUOMBENI RAIS MAGUFULI

MKUU wa Mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka amewataka viongozi wa dini na watanzania kuendelea kumuombea Rais John Magufuli katika jitihada za kurejesha misingi ya maadili, nidhamu na uwajibikaji katika utumishi wa umma iliyoachwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

Amesema katika kipindi cha mwaka mmoja wa utawala wa Rais Magufuli, Serikali ya Awamu ya Tano imejipambanua kwa vitendo katika kupiga vita rushwa, ufisadi, kusimamia nidhamu na miiko ya uongozi katika utumishi wa umma.

Mtaka ameyaeleza hayo jana Jijini Dar es Salaam wakati wa mahojiano maalumu na mwandishi wa habari hizi kuelekea katika maadhimisho ya miaka 55 ya uhuru wa Tanzania Bara.

Mtaka alisema hatua zinazoendelea kuchukuliwa na Rais Magufuli katika kurejesha nidhamu katika utumishi wa umma, ikiwemo mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi ni jambo la kupongezwa, kwa kuwa limelenga katika kuwakumbusha watendaji kuwa uongozi ni dhamana.

Mtaka alisema kiongozi wa umma ni kioo na kiunganishi katika jamii anayoiongoza, hivyo ni wajibu wa kila kiongozi wa umma kujenga taswira chanya ya kiutawala katika kuwahudumia wananchi kwa kutambua kuwa dhamana ya kiongozi ndio tumaini la watawaliwa.

“Katika siku za hivi karibuni tumeshuhudia sekta binafsi zikichukua watumishi waandamizi kutoka serikalini, hiki ni kiashiria kuwa nidhamu na maadili ya kazi yameimarika kwa kiasi kikubwa sana serikalini,” alisema.

Mtaka alisema katika kipindi cha mwaka mmoja wa Serikali ya Awamu ya Tano kuna na mageuzi makubwa katika utendaji na uwazi wa shughuli za serikali, hatua iliyosaidia kuokoa kiasi kikubwa cha fedha kilichokuwa kikipotea katika miaka ya nyuma.
SOURCE HABARI LEO

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

CCM YASHINDA UBUNGE, UDIWANI KWA 100%

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimeshinda kwa asilimia 100 kwenye uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Buyungu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *