Home / Habari za Kimataifa / DOMINIC ONGWEN AKANA MASHTAKA MBELE YA ICC

DOMINIC ONGWEN AKANA MASHTAKA MBELE YA ICC

Kamanda mkuu wa kwanza kabisa wa kundi la Lord’s Resistance Army LRA la nchini Uganda, Dominic Ongwen amekana mashtaka yanayomkabili alipofika mbele ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC mjini Hague.

Ongwen ni mwanajeshi mtoto wa zamani kufunguliwa mashtaka na mahakama hiyo ya kimataifa .

Ongwen ambaye anakabiliwa na makosa 70 ya uhalifu dhidi ya binadamu nchini Uganda, amefunguliwa mashtaka zaidi kuliko mshukiwa yoyote ambaye amefika mbele ya mahakama hiyo.

Dominic Ongwen, alikuwa kijana mdogo wakati alitekwa nyara na kushirikishwa katika shughuli za kundi hilo katili la waasi.

Mwanahabari wa BBC mjini the Hague amesema kesi yake inahusu matatizo mengi aliyosababisha wakati wa vita vilivyosababisha vifo vya zaidi ya watu elfu 100, alikuwa mtoto aliyevalishwa mavazi ya waasi.

_92847533_1a1dfcc1-974f-44b4-a83c-1490e7885e8e

Dominic Ongwen ni nani?

  • Inasemekana alitekwa nyara na kundi la LRA , akiwa na umri wa miaka 10, alipokuwa akielekea shuleni Kaskazini mwa Uganda.
  • Alipanda ngazi na kuwa kamanda mkuu.
  • Alishtakiwa kwa makosa ya uhalifu dhidi ya binadamu na makosa mengine ya kivita, ikiwemo mauaji na utumwa.
  • Mahakama ya kimataifa ya ICC ilitoa kibali cha kukamatwa kwake mwaka 2005.
  • Fununu zilienea kwamba aliuawa mwaka huo huo wa 2015.
  • Marekani ilitoa tuzo ya $5m (£3.3m) kwa yeyote ambaye alikuwa na taarifa kumuhusu mnamo mwaka 2013.

Dominic Ongwen – Wasifu kamili

_92847534_3efedc31-5633-4113-8671-e84d48aaade7

Bwana Ongwen anadaiwa kuongoza shambulio katika kambi nne za wakimbizi wa ndani Kaskazini mwa Uganda, kuwaua na kuwatesa raia, na kuwalazimisha wanawake kuolewa na pia kuwashirikisha watoto vitani.

Alikamatwa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati mwezi Januari mwaka 2015, baada ya kutafutwa na jeshi la Marekani na Afrika tangu 2011.

Uganda ilikubaliana kwamba Bw Ongwen alistahili kuhukumiwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC licha ya kukosa uaminifu kwa mahakama hiyo.

Kundi la LRA, lilianza miongo miwili iliyopita Kaskazini mwa Uganda na linatarajiwa kuwa na wapinganaji kati ya 200-500 wengi wao wakiwa wanajeshi watoto. Kundi hilo linadaiwa kuendesha shughuli zake eneo kubwa kubwa la Afrika ya Kati.

SOURCE BBC SWAHILI

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mbunge Bobi Wine akamatwa Uganda baada ya dereva wake kuuawa

  Boni Wine Mbunge nchini Uganda Robert Kyagulanyi maarufu kama Boni Wine amekamatwa na polisi …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *