Home / Habari za Kimataifa / WALIOMLAZIMISHA MWAFRIKA KUINGIA KWENYE JENEZA WANYIMWA DHAMANA AFRIKA KUSINI.

WALIOMLAZIMISHA MWAFRIKA KUINGIA KWENYE JENEZA WANYIMWA DHAMANA AFRIKA KUSINI.

Wakulima wawili wazungu nchini Afrika kusini wanaolaumiwa kwa kumlazimisha mwanamme mwafrika kuingia kwenye jeneza kwa kupitita shamba lao wamenyimwa dhamana na mahakama.

Mwezi uliopita Theo Martins Jackson na Willem Oosthuizen, walifunguliwa mashtaka ya kuteka nyara na kudhuluma kwa viwango vya kusababisha madhara ya kimwili.

Walikamatwa baada ya video moja ya dakika ishirini ambayo ilirekodiwa tarehe 17 mwezi Agosti kuanza kusambaa mitandaoni ikionyesha mwanamme mzungu akimlazimisha mwanamme mwafrika kuingia kwenye jeneza, akimtishia kumumwagia mafuta na kumchoma.

Taarifa zinasema kuwa mwendesha mashtaka alipinga wawili hao kuachuliwa kwa dhamana akidai kuwa muathiriwa Victor Mlotshwa ametishiwa maisha tangu akamatwe.

Jaji anayesikiliza kesi ametaja kitendo hicho kuwa cha kushangaza na cha kibaguzi na kuongeza kuwa si jambo la kushangaza kuwa ulimwengi ulishtushwa nacho.

SOURCE BBC SWAHILI

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

DSTV, AZAM na ZUKU zatakiwa kuonyesha bure vipindi vya stesheni za Tanzania

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini Tanzania ,Dr.Harrison Mwanyembe Waziri wa Habari, Utamaduni, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *