Home / Habari za Kimataifa / TALAKA TATU MARUFUKU INDIA.

TALAKA TATU MARUFUKU INDIA.

Mahakama moja kaskazini mwa India, imefutilia mbali utaratibu wa dini ya kiislamu wa talaka tatu ambao unampa nafasi mwanamume wa kiislam kumuacha mkewe kwa kusema mara tatu ‘talaka’ na kusema kwamba si utaratibu wa kisheria na ni kinyume cha katiba.

Mahakama kuu ya Allahabad imesema kwamba utaratibu huo umekuwa ukikiuka haki za wanawake wa kiislam .

Mahakama kuu nchini India kwa sasa inaendelea kusikiliza changamoto tofauti zinazotokana na utaratibu huo wa talaka.

Wakosoaji wa mambo wanasema marufuku hiyo inaweza kuwaondoa wanawake wa kiislam katika ufukara.Nchini India ,ndoa katika baadhi ya jamii hutumia sharia za kiislam na baadhi hufuata taratibu na sheria za serikali .

Wafuasi na wanaunga mkono utaratibu huo wa talaka tatu tayari wamesha toa tamko kuwa mjadala huo wa hivi karibuni umewalenga waislamu na kwamba ni kinyume cha haki.

Mjadala unaendela.

SOURCE BBC SWAHILI

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mbunge Bobi Wine akamatwa Uganda baada ya dereva wake kuuawa

  Boni Wine Mbunge nchini Uganda Robert Kyagulanyi maarufu kama Boni Wine amekamatwa na polisi …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *