Home / Habari za Kimataifa / KANYE WEST BADO ATAWANIA URAIS 2020?

KANYE WEST BADO ATAWANIA URAIS 2020?

Kanye West amelejea kwenye Twitter na inaonekana kana kwamba ameamua kuchelewesha nia yake ya kuwania urais Marekani.

Mwanamuziki huyo alikuwa hajaandika ujumbwe wowote kwenye mitandao ya kijamii tangu alipolazwa hospitalini mwezi uliopita.

Kanye aliandika kwenye Twitter kufafanua yaliyojiri kwenye mkutano wake na Donald Trump, ambapo alisema walikutana “kujadili masuala mengi yanayoangazia tamaduni nyingi.”

Mwishoni kabisa, aliandika “#2024”.

Wengi wanaamini alikuwa anagusia mpango wake wa kutaka kuwania urais Marekani.

Alitangaza nia yake mara ya kwanza wakati wa tuzo za video za muziki za MTV mwaka 2015.

Wakati huo, alisema angewania 2020.

Lakini baadhi sasa wanasema ameahirisha mpango wake ili kumpa Trump fursa ya kuwania uras kwa muhula wa pili.

Kanye West majuzi alitangaza kwamba iwapo angepiga kura mwaka huu basi angempigia Bw Trump.

Bw Trump alipokutana na Kanye Jumanne alisema wao ni “marafiki” na kumweleza Kanye kama “mtu mzuri”.

 SOURCE BBC SWAHILI.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mbunge Bobi Wine akamatwa Uganda baada ya dereva wake kuuawa

  Boni Wine Mbunge nchini Uganda Robert Kyagulanyi maarufu kama Boni Wine amekamatwa na polisi …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *