Home / Habari Za Kitaifa / UHARIBIFU WA MAZINGIRA WAKAUSHA VYANZO VYA MAJI KAKONKO.

UHARIBIFU WA MAZINGIRA WAKAUSHA VYANZO VYA MAJI KAKONKO.

WILAYA ya Kakonko mkoani Kigoma inakabiliwa na tatizo kubwa la uharibifu wa mazingira hali inayochangia kuharibiwa kwa vyanzo vingi vya maji kutokana na shughuli za kibinadamu ikiwemo kilimo kufanyika kwenye maeneo hayo.

Mkuu wa Wilaya Kakonko, Kanali Hosea Ndagala alisema hayo katika kijiji cha Mbizi wilayani humo alipoongoza upandaji miti katika bonde la kijiji hicho kufuatia kuhamishwa kwa wananchi waliokuwa wakilima na kufanya shughuli mbalimbali eneo hilo ili kupisha mradi wa maji.

Alisema tangu aingie wilayani humo ameshuhudia mito mingi ambayo ilikuwa ikitiririsha maji mwaka mzima, lakini kwa sasa sehemu kubwa ya mito hiyo ukiwemo mto Muhwazi uliokuwa maarufu kwa kilimo cha mpunga unakaribia kukauka.

Ili kukabiliana na hali hiyo, ametoa mwito kwa watu wote wanaofanya kazi mbalimbali kwenye maeneo ya vyanzo vya maji na hifadhi za misitu kuondoka mara moja na kwamba wale wote watakaokamatwa katika maeneo hayo watachukuliwa hatua kali.

SOURCE HABARI LEO

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

CCM YASHINDA UBUNGE, UDIWANI KWA 100%

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimeshinda kwa asilimia 100 kwenye uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Buyungu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *