Home / Michezo / U-15 kujipima kwa Burundi kesho

U-15 kujipima kwa Burundi kesho

TIMU ya soka ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 15 imerudi juzi toka Zanzibar, ambako ilicheza mechi mbili za kirafiki na kushinda zote.

Akizungumza na gazeti hili jana kocha wa timu hiyo, Oscar Mirambo alisema maandalizi ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Burundi ni mazuri kwani mechi zote za kirafiki walizocheza wameshinda.

Timu hiyo inatarajiwa kucheza na vijana wenzao wa Burundi kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi kesho. Mechi hiyo ni ya kirafiki pia.

“Zanzibar tulicheza michezo miwili na yote tumeshinda kwa idadi kubwa ya mabao kwani mchezo wa kwanza tulishinda mabao 8-1 dhidi ya Kombaini ya Unguja Kaskani na wa pili mabao 16-0 dhidi ya kombaini ya Kusini hivyo ni dalili nzuri kuwa mchezo wa Jumapili (kesho) tutashinda,” alisema Mirambo Timu hiyo ambayo jana ilifanya mazoezi Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, makocha walionekana wakifundisha zaidi kushambulia na kuzuia.

Wapinzani wao timu ya Taifa ya Burundi waliwasili jana kwa ajili ya mchezo huo utakaochezwa Jumapili, Uwanja wa Azam Complex.

Timu hiyo inaandaliwa kwa ajili ya kushiriki michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 20 mwaka 2019 ambapo Tanzania itakuwa mwenyeji.

SOURCE HABARI LEO

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Willian anasema hakuna sababu ingemfanya kusalia Chelsea iwapo Antonio Conte angebakia

Willian alifunga magoli 13 na kutoa pasi 12za usaidizi katika mechi 55 za Chelsea msimu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *