Home / Michezo / JKT Ruvu waitumia salamu nzito Simba

JKT Ruvu waitumia salamu nzito Simba

Licha ya kupokea kichapo cha bao 3-0 kutoka kwa Yanga mwishoni mwa wiki iliyopita, klabu ya JKT Ruvu imeiambia Simba kwamba ijiandae kwani hasira zao zitamalizikia kwa vinara hao wa Ligi Kuu.

Maafande hao wameendelea kujinadi kupitia kwa Msemaji wake, Constantine Masanja kwamba Simba itakuwa na idadi sawa ya wachezaji na timu hiyo.

Masanja ameanza kwa kuelezea mchezo wao dhidi ya Yanga na kumpongeza kocha wa kikosi hicho Bakari Shime.

“Kwanza ninapenda kusema mashabiki wa JKT Ruvu wawe na imani na timu yao, tumeanza vibaya kwa sababu za kiufundi.

” Kushindwa si tatizo tatizo ni kuangalia nini tutafanya kwenye michezo ijayo, mchezo dhidi ya Simba sio mgumu kwa sababu ipo kwenye ratiba yetu, Simba watakuwa na wachezaji 11 na sisi tutakuwa na wachezaji 11″ alisema Constantine Masanja.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Man United iko mbioni kumtangaza Mkurugenzi wa michezo

Golikipa wa zamanI wa Man United Edwin Van De Sar anatajwa kuwa na nafasi kubwa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *