Home / Habari Za Kitaifa / HALIM ASHAULI ZATAKIWA KUVUNA MAJI.

HALIM ASHAULI ZATAKIWA KUVUNA MAJI.

SERIKALI imezitaka halmashauri zianze kuvuna maji ya mvua kwa kujenga mabwawa makubwa na madogo katika maeneo yao, ili kukabiliana na uhaba wa maji utakaosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi.

Halmashauri zote pia zimetakiwa kuhakikisha nyumba za makazi na majengo ya taasisi za umma na binafsi yanayojengwa, katika maeneo ya michoro yake lazima ioneshe miundombinu ya uvunaji wa maji ya mvua.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Gerson Lwenge ametoa maagizo hayo wakati wa ziara kukagua miradi ya maji iliyojengwa na inayoendelea kujengwa katika mkoa wa Rukwa.

Ameagiza kila wilaya ianze kuvuna maji ya mvua kwa kujenga angalau bwawa moja la maji kwa kutumia mapato ya ndani ya halmashauri husika, ili kukabiliana na uhaba wa maji unaoweza kusababishwa na mabadiliko ya tabia nchi.

“Kutokana na mabadiliko ya tabianchi na uharibifu wa mazingira unaosababishwa na shughuli za binadamu katika vyanzo vya maji sasa mito imeanza kukauka na kutishia sehemu mbalimbali za nchi kuwa jangwa, maji chini ya ardhi yamehavipungua sana, visima vinavyochimbwa havina maji ya kutosha, mvua za masika zimeanza kupungua, Wataalamu wapo watumike kuandaa michoro na kufanya usanifu ili wilaya zetu zianze kuvuna maji kwa kujenga mabwawa makubwa na madogo katika maeneo yao,” alisisitiza.

Ametahadharisha kuwa hata migogoro mingi ya wakulima na wafugaji nchini chanzo chake ni uhaba wa maji uliojitokeza katika maeneo mbalimbali huku akikumbusha kuwa tafiti mbalimbali zinatahadharisha vita ya kuu tatu ya dunia itasababishwa na migogoro itakayotokana na ukosefu wa kiwango cha kutisha cha maji.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Zelothe Steven amemweleza Waziri Lwenge kuwa ni aibu kwa mkoa huo unakabiliwa na tishio la kuwa jangwa wakati uoto wake wa asili ni sawa na wa mikoa ya Iringa na Njombe.

SOURCE HABARI LEO.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Historia ya marehemu Isaac Nyagabona Muyenjwa Gamba

HISTORIA YA MAREHEMU ISAAC NYAGABONA MUYENJWA GAMBA. Ratiba Kwa Ufupi Jumatatu Alfajiri – Kupokea Mwili Airport …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *