Home / Michezo / Yanga shughuli nyingine leo

Yanga shughuli nyingine leo

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya soka Tanzania bara, Yanga leo wanashuka dimbani katika mchezo dhidi ya African Lyon utakaochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Huo utakuwa mchezo wa 17 wa ligi, ikiwa tayari imecheza 16, imeshinda 11, imepata sare tatu na kupoteza michezo miwili na ikishika nafasi ya pili kwa pointi 36 nyuma ya vinara Simba yenye pointi 38.

Yanga na Simba zimetofautiana pointi mbili, ambapo sasa zitakuwa zikipokezana kukaa kileleni kama zitaendelea kushinda mechi zao za ligi.

Iwapo Yanga itaifunga African Lyon leo, itapanda kileleni kwa pointi 39, pointi moja mbele ya Simba, lakini inatakiwa kuomba vinara hao kufanya vibaya katika mechi ya kesho dhidi ya JKT Ruvu ili iendelee kubaki kileleni. Yanga inacheza na African Lyon ikiwa na kumbukumbu nzuri ya kuifunga mabao 3-0 katika mchezo wa raundi ya kwanza.

Lyon inashika nafasi ya 12 kwa pointi 18 hivyo ni lazima ipambane kupata matokeo mazuri. Sio mechi rahisi kwa Yanga, kwani African Lyon imekuwa ikizikazia timu kubwa.

Ilitoka sare mara mbili dhidi ya Azam FC katika mchezo wa raundi ya kwanza na wa pili wiki iliyopita. Pia, iliifunga Simba bao 1-0 katika uwanja huo wa Uhuru kwenye mechi ya mzunguko wa kwanza.

Kwa hiyo, utakuwa ni mchezo mgumu kwa kila mmoja, Yanga ikihitaji pointi ili isikae mbali dhidi ya wapinzani lakini pia, African Lyon ikihitaji pointi kujiondoa kwenye hatari ya kushuka daraja.

Yanga huenda leo ikawatumia wachezaji wake wawili iliyowasajili kwenye dirisha dogo Mzambia Justine Zullu ambaye tayari amepata kibali cha ukazi na Mzanzibari Emmanuel Martin aliyetokea JKU. Wachezaji hao walikosekana katika mchezo uliopita dhidi ya JKT Ruvu ambapo Yanga ilishinda mabao 3-0.

SOURCE HABARI LEO

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Willian anasema hakuna sababu ingemfanya kusalia Chelsea iwapo Antonio Conte angebakia

Willian alifunga magoli 13 na kutoa pasi 12za usaidizi katika mechi 55 za Chelsea msimu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *