Home / Habari za Kimataifa / SENEGAL KUONGOZA ”KUPINDULIWA KWA JAMMEH”

SENEGAL KUONGOZA ”KUPINDULIWA KWA JAMMEH”

Awali Jammeh alikubali kushindwa na mfanyabiashara Adama Barrow wakati wa uchaguzi wa Disemba Mosi

Senegal itaongoza hatua za kijeshi kumuondoa madarakani rais wa Gambia Yahya Jammeh ikiwa atakataa kung’atuka wakati kipindi chake kitakapokamilika tarehe 19 mwezi Janauri kwa mujibu wa afisa wa cheo cha juu wa jumuiya ya Ecowas.

“Vikosi vya kijeshi viko tayari kuwapa watu matakwa yao, ikiwa wapatanishi wanaoongozwa na rais wa Nigeria Muhammadu Buhari watashindwa kumshawishi bwana Jammeh kuachia madaraka, alisema Marcel Alain de Souza.

Ameongeza kuwa si matarajio ya Ecowas kuwasha moto eneo hilo na ikiwa bwana Jammeh anapednma watu wake, anahitaji kuondoka madarakani.

Awali Jammeh alikubali kushindwa na mfanyabiashara Adama Barrow wakati wa uchaguzi wa Disemba Mosi, lakini baadaye akaagiza kubadilishwa kwa matokeo akidai kuwa kulikuw na udanganyifu.

SOURCE BBC SWAHILI.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mbunge Bobi Wine akamatwa Uganda baada ya dereva wake kuuawa

  Boni Wine Mbunge nchini Uganda Robert Kyagulanyi maarufu kama Boni Wine amekamatwa na polisi …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *