Home / Michezo / Tanzania yapanda viwango FIFA

Tanzania yapanda viwango FIFA

Kikosi cha Taifa Stars

Shirikisho la Soka Duniani, FIFA limetangaza viwango vipya vya ubora vya mchezo huo kwa mwezi huu ikiwa ni orodha ya mwisho kabisa kwa mwaka huu.

Tanzania imepanda kwa nafasi 4 na kuwa ya 156 katika viwango hivyo katika mwezi ambao haukuwa na mabadiliko makubwa kutokana na uchache wa mechi za kimataifa.

Hakuna mabadiliko katika nafasi kumi za juu Duniani huku Argentina ikiendelea kuwa kinara ikifuatiwa na Brazil na Ujerumani na Chile.

Kwa upande wa Afrika, Senegal imesalia kileleni katika nafasi ya 33 duniani ikifuatiwa na Ivory Coast na Tunisia. Uganda imeendelea kuwa kinara ukanda wa Afrika Mashariki kwa kukamata nafasi ya 72 duniani ikifuatiwa na Kenya katika nafasi ya 89 na Rwanda katika nafasi ya 92.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Man United iko mbioni kumtangaza Mkurugenzi wa michezo

Golikipa wa zamanI wa Man United Edwin Van De Sar anatajwa kuwa na nafasi kubwa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *