Home / Habari za Kimataifa / TUNISIA YAMKAMATA MPWA WA MSHAMBULIAJI BERLIN.

TUNISIA YAMKAMATA MPWA WA MSHAMBULIAJI BERLIN.

IS walitoa kanda ya video ikimuonyesha Amri akilitii kundi hilo

Vikosi vya usalama nchini Tunisia vimemkamata mpwa wa mshambuliaji kwenye soko mjini Berplin, Anis Amri na washukiw wengine wawili.

Wizara ya masuala ya ndani nchini Tunisia, inasema kuwa watu hao wenye umri kati ya miaka 18 na 27 ni wanachama cha kundi la kigaidi.

Mzaliwa wa Tunisia Amri, mwenye umri wa miaka 24, aliuawa kwa kupigwa risasi na polisi karibu na mji wa Milan nchini Italia mapema Ijumaa.

Shambulizi la lori la siku ya Jumamosi kwenye soko, lilisababisha vifo vya watu 12 na kuwajeruhi wengine 49.

Wizara ya masuala ya ndania ilisema kuwa mpwake huyo Amri, alikiri kuwasiana na mjombake kupitia mtandoa wa Telegram ili kukwepa kuchunguzwa.

Inaripotiwa kuwa watatu hao wemekuwa wakihudumu kwenye miji ya Fouchana nje ya mji wa Tunis na Oueslatia karibu na nyumbani kwao Amri, umbali wa kilomita 150 kutoka mji mkuu.

SOURCE BBC SWAHILI.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mbunge Bobi Wine akamatwa Uganda baada ya dereva wake kuuawa

  Boni Wine Mbunge nchini Uganda Robert Kyagulanyi maarufu kama Boni Wine amekamatwa na polisi …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *