Home / Habari za Kimataifa / POLISI 29 WASHTAKIWA KWA KUTAKA KUIPINDUA SERIKALI UTURUKI.

POLISI 29 WASHTAKIWA KWA KUTAKA KUIPINDUA SERIKALI UTURUKI.

Askari waliohusika katika jaribio la mapinduzi nchini Uturuki washtakiwa

Takriban maafisa wa polisi 29 wanashtakiwa mjini Instabul Uturuki kwa kuhusika katika jaribio la mapinduzi mnamo mwezi Julai.

Kesi hiyo ndio muhimu zaidi kuwahi kufanyika huku zaidi ya mashtaka 1000 yakiandaliwa. Huku maafisa wengine 40 wakizuiliwa kesi hiyo inatarajiwa kuwa kubwa zaidi katika historia ya Uturuki ya leo.

Rais wa Uturuki katikati Reccep Tayip Erdogan

Washukiwa wanashtakiwa kwa kuwa na lengo la kuipindua serikali mbali na kujihusisha na kundi linaloongozwa na muhubiri anayeishi Marekani Fethullah Gulen, ambaye mamlaka inamlaumu kwa kupanga njama hiyo.

SOURCE BBC SWAHILI.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mbunge Bobi Wine akamatwa Uganda baada ya dereva wake kuuawa

  Boni Wine Mbunge nchini Uganda Robert Kyagulanyi maarufu kama Boni Wine amekamatwa na polisi …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *