Home / Michezo / Farid sasa kimeeleweka Tenerife

Farid sasa kimeeleweka Tenerife

KIUNGO mshambuliaji wa Azam FC, Farid Mussa anatarajiwa kuondoka nchini leo usiku kuelekea Hispania kujiunga na klabu ya Tenerife ya daraja la pili. Safari ya kiungo hiyo imeiva baada ya Tenerife kumtumia tiketi ya ndege.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffar Idd alisema Farid ataondoka saa 5 usiku kwa ndege ya KLM ambapo atapitia Amsterdam, Barcelona hadi kufika Tenerife na kujiunga na timu hiyo kwa mkopo.

“Kesho (leo) saa 5 usiku Farid ataondoka kwenda Hispania kwa ndege ya KLM kujiunga na timu ya Tenerife inayoshiriki ligi daraja la pili, tayari ametumiwa tiketi kwa ajili ya safari hiyo na sisi Azam tunamtakia kila la kheri katika maisha mapya ya soka,” alisema Jaffar huku akiwaonesha wandishi tiketi hiyo.

Farid anakwenda Tenerife kwa mkopo hivyo Azam FC watakuwa wanamlipa stahiki zote ikiwemo mshahara kwa mujibu wa mkataba walioingia na klabu hiyo.

Awali Tenerife walitaka kumsajili winga huyo kwa mkataba wa moja kwa moja baada ya kufaulu majaribio lakini Azam walikataa baada ya kuwekewa dau dogo mezani na ndio chanzo cha mchezaji huyo kukaa nchini karibu miezi sita bila kujua hatima yake.

Hivi karibuni wadau wengi wa soka walihoji sababu za mchezaji huyo kuendelea kuwepo nchini huku akiwa amefuzu majaribio yake, mmoja wa waliohoji ni Mbwana Samatta anayecheza soka ya kulipwa katika timu ya FC Genk ya Ubelgiji.

Suala hilo lilifanya uongozi wa Azam kuibuka na kudai mchezaji huyo alikwama kutokana na kwamba bado vibali vyake vya kufanya kazi na kuishi Hispania havijawa tayari na kuahidi kulishughulikia. Kuondoka kwa Farid kunaweza kufungua milango kwa wachezaji wengine wa Tanzania kwavile atautangaza vyema mpira wa nchi.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Willian anasema hakuna sababu ingemfanya kusalia Chelsea iwapo Antonio Conte angebakia

Willian alifunga magoli 13 na kutoa pasi 12za usaidizi katika mechi 55 za Chelsea msimu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *