Home / Makala / SIMULIZI YA DUMA ANAVYOTOWEKA DUNIANI.

SIMULIZI YA DUMA ANAVYOTOWEKA DUNIANI.

JAMII ya kimataifa inaamini kabisa kwamba wanyama aina ya duma ambao ni maarufu kutokana na kasi waliyonayo wakiw ahatarini kutoweka kutokana na makazi yao kuvamiwa na binadamu, watanzania bado wana nafasi kubwa ya kuwa kivutio cha wanyama hao kutokana na idadi yao kuwa bado nzuri.

Wakati nasoma taarifa ya kuwapo kwa hatari ya kutoweka kwa wanyama hao ambao inasadikika sasa wapo kiasi cha 7,100 tu duniani, nilichukua simu na kuzungumza na Shelutete wa Tanapa ambaye alinithibitishia kwamba bado wapo wengi tu nchini. Pamoja na uthibitisho huo nilizungumza na Mkurugenzi wa Tawiri, Dk Simon Mduma ambaye naye alikuwa na maneno kuntu kuelezea hali halisi ya duma nchini kwa kuwa tayari wanyama hao wako katika mradi maalumu unaowahusu.

Kwa mujibu wa tafiti iliyoandikwa katika Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC, wanyama hao kwa sasa wapo katika hatari ya kutoweka kutokana na maeneo yao wanayojidai kuvamiwa. Imeelezwa kuwa wanyama hao kwa sasa wamekuwa wakijikuta kila mara wanagombea maeneo yao ya kuwinda na wanadamu. Watafiti wanasema kwamba wanyama hao sasa hivi wanatakiwa kuwekwa katika fungu la wanyama walio hatarini kuweka ili waweze kulindwa.

Kwa mujibu utafiti nusu ya duma wanaosihi sasa wapo katika nchi takaribani sita za Kusini mwa Afrika Aidha imeelezwa kuwa duma wanaoishi katika nchi za Asia ni kwamba wamefutika huku waliobaki ni kama 50 tu na wako Iran. Imeelezwa katika utafiti huo kwamba asilimia 77 ya makazi ya wanyama hawa sasa yako nje ya maeneo yao ya kuwinda ya kawaida yaani hifadhi na mbuga .

Kutokana na shughuli za kilimo zinaozendeshwa na binadamu maeneo ya kuwainda ya wanyama hayo yanaxidi kupungua huku wanyama wanaowindwa na duma wakizidi kutoweka na kumwacha duma katika hali ngumu. Nchini Zimbabwe, duma wamepungua kutoka 1,200 hadi 170 katika kipindi cha miaka 16 kutokana na mabadiliko makubwa ya umiliki wa ardhi uluiosababisha maeneo mengine ya ghifadhi kuangukia katika mgao wa matumizi ya kilimo.

Watafiti wanaamini kwamba tishio la wanyama hawa kutoweka halikuwa katika ajenda za utafiti kwa watu. Hata hivyo wataalamu wamesema kwamba kutokana na tabia ya usiri ya wanyama hao imekuwa taabu sana kukuisanya takwimu zao na hviyio kufanya watafiti kuwasahau na kutojua balaa linawasubiri. Dk Sarah Durant wa Zoological Society of London, Uingereza ambaye ameshiriki kuandika ripoti hiyo amesema kwamba mazingira yanaonesha wazi kwamba mnyama huyo kwa sasa yupo katika hatari ya kutoweka kutokana na kuharibiwa kwa mazingira yake ya kujidai.

Pia kuna shida ya usafirishaji haramu wa duma hasa watoto wake. Matajiri wa nchi za Ghuba ya Ajemi wamekuwa wakitumia fedha zao kupata watoto wa duma na hivyo kuwafanay wanyama haow atoweke kwa kasi katika nyika na mbuga. Imeelezwa kuwa mtoto wa duma anauzwa kwa dola za Marekani 10,000 katika soko la magendo. Kw amujibu wa Mfuko wa kuhifadhi Duma, duniani zaidi ya watoto wa duma 1,200 wamesafirishwa kutoka katika nyika za Afrika kwenda Ajemi katika kipindi cha muongo mmoja uliopita.

Hata hivyo wamesema kwamba asilimia 85 ya watoto haow a duma walikufa wakiwa safarini kwenda kwa matajiri. Imedaiwa na watengeneza ripoti hiyo ya kutoweka kwa duma kwamba hatua za muda mrefu za kuwafanya wanyama hao kuendelea kuwepo ni lazima zichukuliwe sasa kwa kuangalia kwa makini maeneo yanayolindwa kwa ajili ya wanyama hao.

Utafiti unaonesha kwamba ipo haja ya kufanya mabadiliko makubwa katika namna ya kutunza wanyama hao kwa kuwa na mkakati mwingine wa kushirikisha wananchi badala ya kusema tu kwamba wanyama haow apo katika maeneo yanayolindwa au yaliyozuiwa. Dk Kim Young-Overton wa Panthera, anasema kwamba kwa kushirikisha wananchi kutambua umuhimu wa wanyama hao na wao kuwalinda kuliko kutegemea amri tu za hifadhi.

Anasema ipo haja wananchi wakatambua maeneo ambayo wanyama hao huvuinjari na kukaa kutafuta malisho na kuyaheshimu au la tutaendelea kuwaokosa wanyama hawa kwa muda mrefu. Duma nchini mwetu wanaishi katika nyika na aina ya duma wanaopatikana hapa nchini ambao kitaalamu wanaitwa Acinonyx jubatus raineyii akijulikana pia kama duma wa Afrika Mashariki anapatikana pia katika nchi za Kenya, Uganda na Somalia.

Duma nchini Tanzania hupatikana katika maeneo ya Serengeti. Mwaka 2007 idadi ya duma katika nchi za Afrika mashariki walikuwa kati ya 1,960 hadi 2,572 Tanzania ikiwa nchi ya pili kwa kuwa na duma baada ya Afrika Kusini. Tayari duma wametoweka katika maeneo yao ya awali ya Kongo ya kabila, Rwanda na Burundi.

Simulizi hili litaendelea toleo lijalo

SOURCE HABARI LEO.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Chakula cha Wahadzabe cha matunda na nungunungu Tanzania

Jamii ya Wahadzabe ni moja kati ya makabila yaliyobaki duniani yanayoendeleza shughuli za uwindaji, inadhaniwa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *