Home / Habari Za Kitaifa / ZEC: HAKUNA MPASUKO KWA MAKAMISHNA WAKE.

ZEC: HAKUNA MPASUKO KWA MAKAMISHNA WAKE.

MKURUGENZI wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Salum Kassim Ali amesema makamishna wa tume hiyo wanatekeleza na kusimamia majukumu yao bila ya matatizo ambapo Tume ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha na kutoa ripoti ya uchaguzi wa marudio wa Machi 22.

Alisema makamishna wa Tume hiyo ambao wanatoka katika vyama vya siasa vya CCM na CUF hawana malumbano wala mgawanyiko ambapo tangu katika kipindi cha uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 pamoja na uchaguzi wa marudio Machi mwaka huu wanatekeleza majukumu yao bila ya matatizo kwa kufika ofisini kila siku.

Alisema taarifa zinazosemwa mitaani hazina uhalisia na ukweli wa tukio hilo huku zikichukuliwa kisiasa zaidi, kufuatia kauli zilizokuwa zikitofautiana kwa wajumbe hao mara baada ya kufutwa kwa uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 na tume hiyo baada ya kutangazwa na Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salum.

Ali alisema kuwa, ZEC imekamilisha ripoti ya uchaguzi ya mwaka wa marudio wa Machi na inatazamiwa kutolewa mwakani.

Aidha, alisema baada ya Tume ya uchaguzi kufanya vikao vya mikutano mbalimbali pamoja na kupitia majina ya wapiga kura katika daftari la kudumu la wapiga kura, imefuta jumla ya majina 6,747 ambao wamepoteza sifa za kuwa wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi mwengine.

Alisema wapiga kura hao wamefutwa baada ya kubainika wengine kufariki na wengine kuhama katika sehemu moja kwenda nyingine na majina yao kupotea katika daftari la kudumu la wapiga kura.

Alisema marekebisho hayo yamefanywa na Tume ya uchaguzi ya Zanzibar katika vikao vya pamoja vya makamishna kwa lengo la kuleta ufanisi wa kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura ikiwa sehemu ya maandalizi ya uchaguzi wa mwaka 2020.

Mapema, Ali alitumia nafasi hiyo kuvipongeza vyombo ya habari kwa ushirikiano mkubwa uliofanikisha kutoa taarifa za uchaguzi mkuu uliofutwa pamoja na marudio kwa umma.

SOURCE HABARI LEO.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

CCM YASHINDA UBUNGE, UDIWANI KWA 100%

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimeshinda kwa asilimia 100 kwenye uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Buyungu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *